Kuna aina sita za vielezi vya namna:
- Vielezi vya namna halisi
- Vielezi vya namna hali
- Vielezi vya namna vikariri
- Vielezi vya namna mfanano
- Vielezi vya namna viigizi
- vielezi vya namna ala
Vielezi vya namna halisi
Vielezi hivi hutufahamisha jinsi kitendo kinalivyofanyika kwa kutumia maneno halisi bila
kuambatanishwa na maneno mengine au viambishi vingine. Vielezi hivi ni kama vizuri, ovyo,
haraka. Kwa mfano;
Kazija amejikwatua sana.
Wananchi walilia mno.
(b) Vielezi vya namna hali
Ni vile ambavyo hufahamisha hali ambayo kitendo kilifanyika. Vielezi hivi hujihusisha sana na
tabia ya kitu au mtendaji wa kitendo husika. Baadhi ya vielezi hivi ni; kwa furaha, kwa
makini,upesi. Kwa mfano;
Barabara za Bobea zimejengwa upya.
Pwaguzi aliingia kwa makini kwa Kijuba.
(c) Vielezi vya namna vikariri
Vielezi hivi husisitiza tendo lilivyotendwa kwa kutaja kielezi kinachorejelewa mara mbili
mfululizo. Baadhi yavyo ni maneno kama, haraka haraka, ovyo ovyo, juu juu. Kwa mfano;
Maksuudi alilia ovyo ovyo alipompata Maimuna.
Batu alitembea haraka haraka alipoitwa na Bokono.
(d) Vielezi vya namna mfanano
Vielezi vya namna mfanano hutumia KI-mfanano kuelezea kitendo kinavyofanyika kwa
kulinganisha au kumithilisha kitendo hicho na kitu Fulani. Aghalabu, hutumia kiambishi KI – chenye kuelezea namna au jinsi. Kwa mfano nomino mtoto inaweza kuunda kielezi kwa
kuongezewa kiambishi ki- na kuunda kielezi cha mfanano kitoto. Mifano mingine ni kama
jeshi {ki+jeshi} kijeshi
kondoo {ki+kondoo} kikondoo
mifano katika senteszi ni kama vile;
Tamina alipigwa kijeshi.
Zanga alijikaza kisabuni.
(e) Vielezi vya namna viigizi
Vielezi hivi huigiza sauti au mlio wa kitu. Huelezea mlio huo kwa kwa kutumia tanakali za
sauti. Baadhi yavyo ni vielezi kama tuli, chubwi, tifu, chururu vinavyotumika kuelezea milio
tofauti tofauti. Kwa mfano;
Zigu alitulia tuli alipowasili Bokoni
Maimuna alilia kwikwikwi alipoarifiwa kuhusu kifo cha babake.
(f) vielezi vya namna ala
vielezi hivi huonyesha kifaa au kitu kilichotumiwa kutekeleza jambo fulani k.m.
Mlinzi alimuua mwizi kwa sime
Daktari alimdunga maria kwa sindano