Vihusishi vimegawika katika makundi tisa makuu. Nayo ni;
· Vihusishi vya Mahali

Vihusishi hivi hujulisha uhusiano uliopo kati na nomino na mahali. Kwa mfano; mbele ya,
nyuma ya, chini ya, kando ya, karibu na, mbali, mbele ya,ndani ya, na n.k
Kwa mfano;
Gari liliegeshwa kando ya barabara.

Ameketi chini ya mti
· Vihusishi vya Wakati
Hivi kwa upande mwingine huonyesha uhusiano uiopo baina ya tuko na muda au wakati wa
kutendeka. Baadhi ya vivumishi hivi ni kama; baada ya, kabla ya,baada ya, tangu,mnamo n.k
Kwa mfano;
Ni vizuri kusali kabla ya kula chakula

Walikesha hadi usiku wa manane

Mwalimu aliwasalimia wanafunzi kabla ya kuketi

Nlienda baada ya kumuaga mwanangu.

Vihusishi vya kinyume

Kihusushi cha kinyume huonyesha uhusiano wa kinyume. mifani ni kama; licha ya,badala ya, bila n.k.

mifano katika sentensi;

Alifuzu vyema kwenye mtihani wa kitaifa licha ya kukosa kuhuduria shule vyema.

Alienda shambani badala ya soko.

Alivamiwa na majangili na kuuwawa bila sababu

Vihusushi vya kufananisha

Hivi huonyesha uhusiano kwa kufananisha kitu kimoja na kingine. k.m. mithili ya, tamthili ya, kama, mfano wa n.k.

mifano katika sentensi;

Anasoma bibilia kama kasisi

Mwizi alipigwa mithili ya mbwa koko

Salomi ana bidii mfano wa mchwa

Vihusishi vya a- unganifu

Vihusishi hivi huundwa kwa mzizi wa ‘a’ wa uhusiano. Vihusishi hivi huwa na maana mbalimbali kama vile;

i) umilikaji

Mfano; Gari la mwalimu lilioshwa jana,Mahali pa dawa ni pale , vitabu vya wanafunzi viko pale.

ii) Aina / hali ya kitu

Mifano;chakula cha mchana ni kizuri, Uwindaji wa wanyama pori ulipigwa marufuku,

Kihusishi ‘na’ cha mtenda

Kihusishi hiki huonyesha uhusiano kati ya kitendo na mtendaji.

Mifamo; Mgonjwa ametibiwa na daktari, Mtoto amepigwa na babake, Watoto wamenunuliwa pipi na mama

Vihushishi vya sababu

Vihusishi hivi hutumiwa kuonysha uhusiano kati ya kitendo na mtendaji.

Mifano: kwa kuwa, kwa sababu, kwa vile n.k.

Tumeanza kusoma kwa sababu mitihani imekaribia, Ujambazi umepungua kwa kuwa polisi wamimarisha doria, Simwoni kwa vile amejificha.

Vihushishi vilinganishi / Vya ulinganifu

Vihusishi hivi huhusisha vitu kwa kuvilinganisha. mifano: Maria anacheza vizuri kuliko Joshua,shule ni nzuri kushinda nyumbani.

Vihisishi vya kuonyesha hali

Vihusishi hivi hutumiwa kuonyesha hali.

mifano; sawa na, kwa niaba ya,miongoni mwa,kwa minajili ya n.k.

Nitamtembelea kwa minajili ya kwa kumjulia hali, Nililima shamba kwa niaba ya kakangu

Aina za Maneno
Nomino-N
Kiwakilishi-W
Kivumishi – V
Kitenzi-T, Ts au t
Kielezi-E
Kiunganishi – U
Kihisishi – I