- Vishazi tegemezi virejeshi
Ni vishazi vinavyotumia virejeshi ‘-amba’ au ‘o’ ili kuvumisha nomino
kwa mfano: Gari ambalo lilinunuliwa litauzwa sokoni kesho
mto uliofurika mwaka jana ulitatiza wasafiri sana
- Vishazi tegemezi vya masharti
Ni vishazi ambavyo huonyesha dhana ya utegemezi kwa kutumia viambishi ‘-nge-’, ‘-ngali-’,’-ngeli-’ na ‘ki’ na aghalabu hutumia viunganishi ya masharti kama vile ‘kiwa’ endapo, na iwapo kwa mfano:
Ukisoma kwa bidii urafaulu maishani.
Ikiwa nitampata maria mitamwambia
Angelisoma kwa bidii angelipita mtihani.
- Vishazi tegemezi vya kuonyesha kinyume au kasoro
Hivi ni vishazi ambavyo hutumia viunganishi vya kuonyesha kinyume
K.m vile licha ya, japo,ijapo,ijapokuwa n.k.
k.m. Alimwadhibu ingawa hakuwa na makosa.
Ingawa mshahara wake si mkubwa anaikimu familia yake
- Vishazi tegemezi vya kuonyesha sababu
Huundwa kwa viunganishi vya sababu kama vile; kwa sababu, kwa kuwa, kwa vile
kwa mfano; Alikimbia shuline kwa sababu alikuwa amechelewa
Alitembea kwa miguu kwa kuwa kulikuwa na uhaba wa magari
- Vishazi tegemezi vya wakati
Vishazi hivi huonyesha wakati wa kutendeka kwa jambo na hutumia vihusishi vya wakati kama vile; tangu, baada ya, kabla ya na kiambishi ‘po’
kwa mfano;
Tulipoingia kwake alitukaribisha kwa furaha
Alisalimu amri baada ya kuvumaniwa na walinda usalama
- Vishazi tegemezi vya namna au jinsi
Huonyesha namna kitendo kilivyofanyika na hutumia kirejeshi ‘o’
kwa mfano:
Ulivyokuwa ukicheza jana ulitufurahisha
ulivyokuwa unakula jana ulituogofya
- Vishazi tegemezi vya mahali
huonyesha mahali ambapo kitendo kilitendeka . vishazi katika karegoria hii hutumia viambishi PO-KO-MO
kwa mfano:
Alikosomea ninapajua
Alimoingia napajua vizuri
- Vishazi Viambata
Ni vishazi vinavyoundwa kwa vishazi huru viwili vikiwa vimeunganishwa k.m. Baba analala na mama anapika.
Vishazi tegemezi vipo vya aina mbili kutokana na majukumu yake kimuundo
A. Kishazi tegemezi kivumishi (V)
Kishazi tegemezi kivumishi hufanya kazi ya kuvumisha nomino katika tungo.
Mfano; Baba anayenijali
Mbwa aliyepotea
Mwanafunzi aliyefariki
Uliyemuona pale
Aliyempenda sana
B. Kishazi tegemezi kielezi (E)
Kishazi hiki hufanya kazi ya kueleza tendo katika tungo na hujitokeza kueleza dhima tofauti tofauti kama ifuatavyo:-
- Kueleza mahali tendo linapofanyika. Mfano; Alipoingia (mahali dhahiri), Alimochungulia (ndani ya kitu Fulani), Alikoelekea (mahali pasipo dhahiri)
- Kueleza wakati wa tendo. Mfano; Tulipotoka, Alipomchapa, Walipomsema n.k.
- Kueleza masharti katika tendo. Mfano; Akirudi, Angekuja, Angelimpiga, Angalijua n.k.
- Kueleza namna tendo linavyofanyika. Mfano; Alivyoimba, Walivyopendeza, Tulivyomsifu.
- Kueleza kasoro katika kukamilisha tendo. Mfano; Ingawa amesoma, Licha ya kufaulu, Japokua amependekezwa.
- Kueleza sababu ya kufanyika kwa tendo. Mfano; Kwa sababu alipendeza, Kwa kuwa hujafaulu, Kwa vile umenisomesha.
Zoezi
Bainisha Vishazi Katika Sentensi Zifuatazo
- Mwalimu amewasili.
- Amina ambaye ni daktari atakuja.
- Ametajirika japo hakupata elimu.
- Mwalimu anafundisha na wanafunzi wanaandika.
- Tumeanzisha shirika ili tunyanyue hali zetu.