Kiwakilishi ni neno au Kiambisihi kinacho simamia nomino pale ambapo haitajwi. kiwakilishi pia hiutwa Kijina au Kibadala.

Viwakilishi vya Nomino ni maneno yanayotumika badala ya nomino. Kiwakilishi hakiwezi
kuambatanishwa na nomino inayorejelewa. Kuna aina tisa ya viwakilishi navyo ni:

  1. Viwakilishi vya Nafsi
  2. Viwakilishi viashiria
  3. Viwakilishi visisitizi
  4. Viwakilishi vya sifa
  5. Viwakilishi vya idadi
  6. Viwakilishi viulizi
  7. Viwakilishi vimilikishi
  8. Viwakilishi virejeshi
  9. Viwakilishi vya A- unganifu.


Viwakilishi vya Nafsi
Viwakilishi hivi hutumika kwa niaba ya nafsi kwa umoja na kwa wingi.
k.m: mimi, wewe, yeye, sisi, nyinyi, wao

NafsiUmojawingi
Nafsi ya kwanzamimisisi
Nafsi ya piliweweNyinyi/ninyi
Nafsi ya tatuyeyewao

Sisi tuliwatangulia nyinyi kufika hapa.
Mimi si mjinga kama vile yeye anavyofikiria
Viwakilishi Visisitizi
Husisitiza nomino inayowakilishwa kwa kurudiarudia kiashiria chake.
k.m: yuyu huyu, wawa hawa, kiki hiki, papo hapo, mumu humu,
Viwakilishi vya Sifa
Husimama badala ya nomino kwa kurejelea sifa yake.

k.m: -eupe, -zuri, -tamu, -embamba, -rembo, safi
Vyekundu vimehamisha
Warembo wamewasili.
Kitamu kitaliwa kwanza.
Viwakilishi vya Idadi
Hutumika kusimama badala ya nomino kwa kurejelea idadi yake.Vivumish vya idadi ni vya aina mbili:
a) vivumishi vya idadi Kamili- hutumia nambari kuelezea idadi ya nomino. k.m: saba, mmoja, ishirini
Wawili wamepigwa risasi polisi leo jioni.
Alimpatia mtoto wake hamsini kununua chakula
b) Vivumishi vya idadi Isiyodhihirika- huelezea kiasi cha nomino kwa ujumla, bila kutaja idadi kamili
k.m: chache, nyingi, kadhaa, kidogo, wastani
Tutazungumza na wachache kabla ya kuanzisha maonyesho yetu.
Kadhaa zimeripotiwa kupotea.

Viwakilishi Viulizi
Viwakilishi viulizi hutumika kwa niaba ya nomino katika kuulizia swali.Baadhi ya viwakilishi viulizi huchukua viambishi vya ngeli
k.m: -ngapi?, -pi?
Vingapi vinahitajika? – kuulizia idadi
Zipi zimepotea?
Kunavyo viwakilishi viulizi vingine ambavyo havichukui viambishi vyovyote.
k.m: wapi?, gani?, nini?, vipi?
Gani imefunga bao hilo?
Wapi hapana majimaji?
Yule mvulana alikupatia nini?
Uliongea naye vipi? – kuulizia namna
Viwakilishi Vimilikishi

Viwakilishi hivi hurejelea nomino kwa kutumia vimilikishi. k.m: -angu, -ako, -ake, -etu, -enu, -ao
Kwetu hakuna stima.
Lake limekucha.
Zao zimeharibika tena
Viwakilishi Virejeshi (O-Rejeshi)
Hutumia O-rejeshi kurejelea na kusimamia nomino
k.m: ambaye, ambao, ambalo, ambacho, huyo, yule
Ambalo lilipotea limepatikana.
Ambaye hana mwana, aeleke jiwe
Viwakilishi Vya A-Unganifu
Huwakilishi nomino kwa kutaja kinachomiliki nomino hiyo. Huundwa kwa kuambatanisha
kiambishi cha nafsi/ngeli pamoja na kiambishi -a cha a-unganifu, kisha nomino nyingine
k.m: cha, la, kwa, za, ya
Cha mlevi huliwa na mgema
Za watoto zitahifadhiwa.

Aina za Maneno
Nomino-N
Kivumishi – V
Kitenzi-T, Ts au t
Kielezi-E
Kiunganishi – U
Kihusishi – H
Kihisishi – I