Katika lugha ya Kiswahili Kuna angalau aina nane za maneno ambazo wataalamu wengi wa lugha hukubaliana nazo. Katika mada hii utaweza kujifunza na kubainisha aina zote nane za Maneno na jinsi zinvyotumika katika sentensi. Utaweza pia kujifunza namna ya kutofautisha aina za maneno; neno ni nini?
(a) Neno ni mkusanyiko wa silabi ambazo huletwa pamoja kwa utaratibu fulani ili kuleta maana inayokusudiwa.
(b) Neno ni mkusanyiko wa sauti zinazotamkwa au kuandikwa pamoja na kuleta maana.
(c) Neno ni umbo la lugha lenye maana lililoundwa na sauti au herufi kadha. Kwa mfano: Neno mama limeundwa na sauti /m/, /a/,/m/na/a/ na linamaanisha mzazi wa kike.
Lugha ya Kiswahili inazo aina nane za maneno. Nazo ni:
- Nomino-N
- Kiwakilishi-W
- Kivumishi – V
- Kitenzi-T, Ts au t
- Kielezi-E
- Kiunganishi – U
- Kihusishi – H
- Kihisishi – I
Nomino – N
Nomino ni neno linalotaja mtu, kitu, mahali,
hali au jambo fulani.Mifano katika sentensi:
(a)Kevin na Njoroge wameandikiana barua.
(b) Nairobi ni mji mkuu wa Kenya.
(c) Tulifurahishwa na kuimba kwake.
(d)Woga wao uliwasababishia kukosa usingizi.
(e) kitabu kipya kimewekwa juu ya meza.
Aina za nomini; kuna aina sita za nomino
- Kiwakilishi (W)
Kiwakilishi ni neno linalotumiwa kusima mia nomino pale ambapo nomino husika
haijatajwa.Mifano katika sentensi:
(a) Wake ampendaye yu pale.
(b) Wewe na mimi tutaandika barua.
(c) Yote yayamwagwa chini.
(d) Wale watanunuliwa viatu vipya.
(e) Hikikilinunuliwa na yule.
Aina ya viwakilishi;Kuna aina tisa ya viwakilishi
- Kivumishi (V)
Kivumishi ni neno linalotumiwa kutoa taarifa
zaidi kuhusu nomino au kiwakilishi.Mifano katika sentensi:
(a) chai yote imemwagika.
(b) Gari lake limepotea.
(c) Farasi wachache wamenunuliwa.
(d) Gari lili hili ni langu.
(e) Kifaa hiki ni kipya.
Aina ya vivumishi; kuna aina kumi na moja ya vivumishi
4, Kitenzi (T, Ts, t)
Kitenzi ni neno linaloashiria kitendo.
Mifano katika sentensi:
(a) Mtoto huyu ni Maria.
(b) Kamau analia sana.
(c) Waziri Ametembea haraka sana.
(d) Juma aliandika barua inayovutia.
Aina za vitenzi; kuna aina tano kuu za vitenzi
- Kielezi (E)
Kielezi ni neno linalotumiwa kufafanua kivumishi, kitenzi au hata kielezi kingine.
Mifano katika sentensi:
(a) Mwanafunzi mwerevu sana ametuzwa.
(b) Mwanafunzi amepigwa vibaya.
(c) jambazi huyo ameuawa kinyama
(d) Mwanafunzi ameandika barua vizuri.
(e) Askari jeshi anatembea polepole.
Aina za vielezi; Kuna aina tano za vielezi
- Kiunganishi (U)
Kiunganishi ni neno linalotumiwa kuleta vipashio vya lugha kama vile maneno na
sentensi pamoja.Mifano katika sentensi:
(a) Mimi na wewe tumetoka shuleni
(b) Yuhana anasoma ilhali Maria anacheza.
(c) Juma anafundisha huku wanafunzi wakiandika.
(d) Ningewasaidia lakini mumenipuuza.
- Kihusishi (H)
Kihusishi ni neno linalotumiwa kuonyesha uhusiano uliopo baina ya vipashio vya lugha
kama vile maneno na hata sentensi.Mifano katika sentensi:
(a) mbwa yu juu ya kiti.
(b) Mtoto amepigwa na baba yake vibaya.
8. Kihisishi – I
Kihisishi ni neno linalotumiwa kuonyesha hisia za ndani za mtu. Hisia hizi zinaweza kuwa za furaha, huzuni, masikitiko, uoga, mshangao, majuto, hasira miongoni mwa nyingine.
Mifano katika sentensi:
(a) La! Sitaki kusikiliza upuuzi wako tena.
(b)Maskini! Mama yangu aliendelea kuugua.
(c) Wamama wote, hoyee! Hoyee!
(d) Aka! anasema ataongoza makanamano dhidi ya serikali
(e) Huraa! Tumeshinda.