Nomino ni neno linalotaja mtu,kitu, mahali, hali, au hata jambo fulani. Kuna ina sita za nomino za kiswahili.Nazo ni:
- Nomin za pekee.
- Nomino za jamii/ makundi.
- Nomino dhahania.
- Nomino za wingi.
- Nomino za kawaida.
- Nomino za kitenzi jina.
Nomino za Kawaida
Haya ni majina ya kawaida yanayoweza kutumiwa kurejelea vitu mbalimbali, watu, wanyama,
mahali na kadhalika. Nomino hizi zinaweza kuwa katika umoja au wingi kulingana na ngeli
yake.
k.m: nyumba, mbuzi, daktari, soko, kalamu, jua
Nomino za Kipekee
Haya ni majina maalum ya watu, mahali, bidhaa, kampuni, na kadhalika. Herufi ya kwanza ya
nomino hizi huwa ni herufi kubwa. Nomino za kipekee haziwezi kubadilika, na hivyo basi
hazina wingi.
tanbahi: nomino hiz huitwa za pekee kwa sababu vitu vinavyotajwa huwa na upekee wake kwa sababu hakuna vingine vinavyoitwa hivyo au vyenye sifa zinazofanana na vitu hivi.
k.m: Tanzania, Nairobi, Anita, Athi, Kimbo,
Nomino za Jamii
Nomino za jamii hurejelea kundi la vitu au wanyama, kwa ujumla. Aghalabu vitu
vinavyorejelewa hutokea kwa makundi ya vitu mbili au zaidi. Nomino hizi hutumia wingi tu
tunaporejelea makundi zaidi ya moja.
k.m: jozi la viatu, umati wa watu, bustani la maua, bunga la wanyama
Nomino za Wingi
Nomino hizi hurejelea vitu ambavyo hutokea kwa wingi na haziwezi kuhesabiwa. Vitu kama
hivyo hutumia aina nyingine ya vipimo ili kurejelea kiasi chake. Nomino za wingi hazina umoja.
k.m: maji, maziwa, changarawe, pesa, nywele
Nomino za Vitenzi Jina
Nomino hizi huundwa kutokana na vitenzi kwa kuongeza kiungo KU mwanzoni mwa mzizi wa
kitenzi.
k.m: kulima, kuongoza, kucheza, kulala
Nomino za Dhahania
Haya ni majina ya hali au vitu ambavyo havionekani wale haviwezi kushikika.
k.m: upendo, furaha, imani, elimu, ndoto, mawazo, maisha, usingizi
Aina za Maneno |
Kiwakilishi-W |
Kivumishi – V |
Kitenzi-T, Ts au t |
Kielezi-E |
Kiunganishi – U |
Kihusishi – H |
Kihisishi – I |