Sentensi ni fungu la maneno linalojitosheleza kimaana linalotumiwa katika mawasiliano. sentensi pia inaweza fasiriwa kuwa ni Sentensi huwa ndio ngazi ya juu zaidi katika tungo na hujengwa kwa vishazi.
Sifa za sentensi
- Huwa na ujumbe uliokamilika.
- Huwa na mpangilio maalum wa maneno.
- Huwa na muundo wa kiima na kiarifu.
Aina za sentensi
i) Sentensi Sahili
sentensi sahili ni sentensi rahisi au nyepesi au sentensi yenye wazo moja kuu au kishazi kimoja tu.
Sifa za sentensi sahili
- Huwa fupi.
- Aghalabu huwa na kitenzi kimoja pekee.
- Huwasilisha dhana moja.
- Yaweza kuwa ya neno moja au zaidi.
- Yaweza kuwa na kiima kilichododoshwa.
Kwa Mfano:
- Wanajiandaa.
- Watoto wawili wanaelekea uwanjani.
- Gachiku ni msichana mtiifu.
- Alisoma kitabu cha hadithi
- Sentensi Ambatano
sentensi ambatano amboyo ni sentensi sahili mbili zimeunganishwa kwa kutumia kiunganishi, huwa na vitenzi vikuu viwili na huwasilisha mawazo mawili.
Sifa za sentensi ambatano
- Huwa na vishazi huru viwili.
- Huwa na kiunganishi.
- Huwa na vitenzi viwili au zaidi.
- Hutoa zaidi ya wazo moja.
- Yaweza kuwa na viima vilivyododoshwa.
Kwa mfano:
Sentesi sahili | sentensi ambatano |
Baba amefika nyumbaniBaba amelala | Sentensi hizi mbili sahili zikiunganishwa itakuwa:Baba amefika nyumbani na kulala |
Mwanafunzi amepita mtihaniMwanafunzi hakusoma kwa bidii | Sentensi hizi mbili sahili zikiunganishwa itakuwa:Mwanafunzi amepita mtihani ingawa hakusoma kwa bidii |
Joy amejipamba vizurimariam amejipamba vizuri | Sentensi hizi mbili sahili zikiunganishwa itakuwa:Joy na Mariam wamejipamba vizuri |
Sentensi Changamano
Ni sentensi ambayo huwa na kishazi tegemezi kilichochopekwa ndani.
sentensi changamano huwa na vishazi viwili; kimoja huru na kingine tegemezi. Huwasilisha wazo moja kwa kishazi huru.
*Kishazi ni sehemu ambayo ina kitenzi katika sentensi. Pia yaweza kutambulishwa kwa ‘O’ rejeshi,’amba’,viunganishi na kiambishi ‘po’.
Sentensi changamano huundwa kwa kuunganisha kishazi huru pamoja na kishazi tegemezi, sentensi mbili kwa kutumia o-rejeshi,amba au viunganishi na kiambishi ‘po’
Kwa mfano:
Vishazi | Sentensi ambatano |
Karim amenilitelea Kalamu. Nilikuwa nimetafuta kalamu hiyo kwa muda mrefu. | Karim ameniletea kalamu mbayo nilikuwa nimeitafuta kwa muda mrefu. |
Tunda limeozatunda alililonunua jana | Tunda alilonunua jana limeoza. |
Mwizi aliiba pesaPesa zilizokuwa kabatini | Mwizi aliiba pesa zilizokuwa kabatini. |
Yeye ni mwizi. Alipigwa jana jioni. | Yeye ndiye mwizi aliyepigwa jana jioni. |
Sifa za sentensi changamano
- Huwa na kishazi tegemezi chenye kitenzi kinachovumisha nomino kwa kuirejelea.
- Huwa na kishazi huru kimoja au zaidi.
- Huwa na virejeshi (amba na O) au –enye.
- huweza kuwa na kiunganishi na kiambishi ‘po’
Sentensi tata
Mbali na aina hizi tatu za sentensi, kuna aina ya nne ya sentensi ijulikanayo kama sentensi tata (ambiguous sentence in English) hii huwasilisha dhana au maana zaidi ya moja katika lugha ya Kiswahili. Kwa mfano.
Maria alimpigia Fatuma simu. Mwanafunzi kuna dhana nne katika sentensi hii, unapojibu, jibu hivi;
1.aliwasiliana naye kwa simu
2.alimwadhibu kwa kutumia simu kama kiboko
3..alipiga simu kwa niaba ya Maria.
4.alimwadhibu sababu ya simu.