AINA ZA SENTENSI KIMAANA NA KIUAMILIFU

Kuwepo kwa aina tofauti za sentensi katika lugha inawezesha matumizi yake kwa ufanisi na kwa njia ambayo inaeleweka vizuri na wasemaji wengine. : tutaangazia aina za
sentensi kimaana na kiuamilifu.


Aina za sentensi kimaana


Kwa kuzingatia kigezo hiki, tunapata aina zifuatazo za sentensi:

  1. Sentensi tatanishi.
  2. Sentensi ya masharti.
    • Sentensi tatanishi
      Sentensi tatanishi ni sentensi yenye maana zaidi ya moja. Huwa na maana mbili au zaidi.
      Mifano ya sentensi tatanishi ni:
      (a) Mama amenunua mbuzi.
      Maana:
      (i) Mama amenunua mnyama.
      (ii) Mama amenunua kifaa cha kukunia nazi.
      (b) Nimeona kaa.
      Maana:
      (i) Nimeona mnyama wa baharini mwenyegamba.
      (ii) Nimeona kipande cha kuni kilichochomwa.
      (c) Nancy alimpigia mtoto mpira.
      Maana:
      (i) Nancy alimpiga mtoto kwa kutumia mpira.
      (ii) Nancy alimpiga mtoto kwa sababu ya mpira.
      (iii) Nancy alipiga mpira kwa sababu ya mtoto.
      (iv) Nancy alielekeza mpira kwa mtoto.
      (d) Mamake Kamau na Omondi walitutembelea.
      Maana:
      (i) Walikuja kutembea kwetu/walituzuru.
      (ii) Walitembea badala/kwa niaba yetu.

Sentensi ya masharti
Sentensi ya masharti ni sentensi inayoonyesha kutegemeana kwa matendo au hali.
Sentensi hii hutambulika kutokana na kuwepo kwa viambishi na maneno yafuatayo:
nge, ngali, ngeli, ki, iwapo, ikiwa, kama n.k.
Mifano:

  1. Ukinitusi nitakuzaba makofi.
  2. Atakusamehe ikiwa utaomba msamaha.
  3. Mngalijitahidi mngalifanikiwa maishani.
  4. Angekuja mapema angeniona.
  5. Mvua ikinyesha mapema tutapata faida.
  6. Mithika angalisoma kwa bidii angalifaulu.

Aina za sentensi kiuamilifu


Sentensi za Kiswahili zinaweza kuanishwa kiuamilifu. Yaani, kwa kuzingatia kazi
inayotekelezwa na sentensi ainati za Kiswahili, tunaweza kupata aina mbalimbali
za sentesi. Nazo ni:
(a) Sentensi za taarifa.
(b) Sentensi za maswali/ulizi.
(c) Sentensi za amri.
(d) Sentensi za rai au ombi.
(e) Sentensi za mshangao/kustaajabu.
(a) Sentensi za taarifa
Sentensi za taarifa ni zile ambazo hutoa ujumbe au habari; hujuza kuhusu jambo
fulani.
Mifano:

  • Wewe utakwenda sokoni.
  • Unywaji wa pombe unahatarisha maishayako.
  • Baba atasoma gazeti kesho.
    (b) Sentensi za maswali/ ulizi
    Sentensi za maswali ni sentensi ambazohulenga kupata taarifa au ujumbe fulani.
    Sentensi hizi huhoji au hudadisi ili kupata ujumbe fulani.
    Mifano:
  • Kwa nini umenitusi?
  • Mwalimu atatufunza nini kesho?
  • Mbona Kariuki alianza kuvuta kasumba?
  • Mwalimu wetu wa Kiswahili alihamia shule gani?
  • Ni nani aliyechimba shimo hilo?
    (c) Sentensi za amri/amrishi
    Sentensi za amri ni zile ambazo hulenga
    kumwagiza mtu atekeleze jambo fulani bila hiari yake. Ni sentensi ambazo hulenga kumlazimisha au kumshurutisha mtu afanye jambo fulani,
    Mifano:
  • Andikeni insha hii!
  • Ondoka hapo!
  • Waite watoto!
  • Washa moto tupike sima!
    Usipitie hapa!
    (d) Sentensi za rai/ombi
    Sentensi hizi hulenga kutoa ujumbe wa kutaka usaidizi. Hutoa dhana ya kutaka
    kusaidiwa katika jambo fulani. Ni sentensi ambazo hulenga kumsihi mtu atekeleze au afanye jambo fulani.
    Mifano katika sentensi:
  • Naomba unisaidie.
  • Tafadhali niongezee nyama.
    (e) Sentensi za mshangao/ kustaajabu
    Hizi ni sentensi zinazoonyesha hisia za kuduwaa kutokana na jambo fulani.
    Mifano:
  • Salaale! Paka amemuua nyoka mkubwa!
  • Lo! Kiplang’at ameanguka vibaya!
  • Aka! Kwani mnagombana kila wakati!
    Nyumba iliyojengwa juzi imebomolewa!

Leave a Reply

scroll to top