Kuna wananadharia wanaosema kuwa silabi inaweza kuwasilishwa kwa namna mbalimbali. Pike na Pike (1943) wanasema kuwa muundo wa silabi una matawi na darajia. Baadhi ya wanataaluma wanaona kuwa silabi ina mwanzo na kilele. Wengine hudai kuwa silabi ina upeo na ukingo/mpaka/margin (sehemu ya mwanzo au ya mwisho wa silabi. Kuna wanazuoni wengine kama vile Halle, Harris na Vernaud wanasema kuwa silabi ina vitamkwa vinavyobeba sifa bainifu. Aidha, silabi zenye matawi na darajia zina tia.
Katamba (1996:176) anasema kuwa suala la kuainisha silabi kwa vigezo huru na funge ni la kimapokeo ama kijadi. Hivyo basi tunatakiwa kuangalia silabi husika kama ni nzito au nyepesi.
SILABI NZITO
Ni ile silabi ambayo upeo wake una tawi linalogawanyika.
Kwa mfano;
Mwanzo wa silabi upeo wa silabi ah
l
Kiini cha silabi ukingo wa silabi
a h
SILABI NYEPESI
Ni ile silabi ambayo upeo wake haugawanyiki kwa mfano ba, ma da ,fa ja n.k.
6
Mwanzo wa silabi upeo wa silabi
M a
Mwanzo wa silabi ndio una msukumo wa matamshi. Hivyo basi silabi ma ni huru ni ni nyepesi kwani haina tawi linalogawanyika.
Kila lugha ina muundo wake wa silabi kulingana na idadi ya fonimu zilizopo.
MUUNDO WA SILABI HURU ZA KISWAHILI
Muundo wa irabu pekee kwa mfano katika ua, oa, au
Muundo wa nazali pekee kwa mfano katika mganga, mtoto, mdogo
Muundo wa konsonanti na irabu kwa mfano katika kaka, dada, debe, baba, raha
Muundo wa konsonanti konsonanti na irabu kwa mfano
(a) Kipasuo+kiyeyusho+irabu kwa mfano, pweke
(b) Kikwamizo+kiyeyusho+irabu kwa mfano, swaga
(c) King’ong’o|+kiyeyusho+irabu kwa mfano. Mwaka
(d) Kikwamizo+kipasuo+irabu kwa mfano spika
(e) Kipasuo+kiyeyusho+irabu kwa mfano, bweka
Konsonanti konsonanti kiyeyusho na irabu kwa mfano;
(a) Nazali+kipasuo+kiyeyusho+irabu kwa mfano pingwa
(b) Nazali +kipasuo+ kiyeyusho+irabu kwa mfano pandwa, undwa
(c) Nazali+ kikwamizo+kiyeyusho+irabu kwa mfano chinjwa
MUUNDO WA SILABI FUNGE
Aina hizi za silabi haziishii na irabu. Pia huwa hazisikiki na huweza kutokea mwanzoni, katikati au mwishoni mwa neno
MWANZONI MWA NENO
1. Silabi zenye ukingo /l/ kwa mfano
Alfajiri, almasi, halmashauri, hulka n.k.
2. Silabi zenye ukingo /s/ kwa mfano
Askari, askofu, desturi, mustarehe, rasmi, hospital, taslimu, wastani n.k.
3. Silabi zenye ukingo /k/ kwa mfano
Daktari, bakshishi, iktisadi, takribani, aksante, maksai, muktadha, nuksi, nukta n.k.
4. Silabi zenye ukiongo /r/ kwa mfano
Ardhi, karne n.k.
5. Silabi zenye ukingo /n/ kwa mfano
Ankra
6. Silabi zenye ukingo /m/ kwa mfano
Hamsini, mamsapu, alhamudullilah, hamsa n.k.
7. Silabi zenye ukingo /p/ kwa mfano
Aprili, kaptula, kapteni
8. Silabi zenye ukingo /b/ kwa mfano
Biblia, kabla, rabsha n.k.
9. Silabi zenye ukingo /j/ kwa mfano;
Majhununi
SILABI ZENYE UKINGO ZINAZOTOKEA KATIKATI YA NENO
Kwa mfano, mfalme, daftari, eropleni n.k.
SILABI ZENYE UKINGO ZINAZOTOKEA MWISHONI MWA NENO
Kwa mfano jehanam, inshallah n.k.
Kwa ujumla maneno mengi yanayotumia silabi funge mengi ni ya kukopa.
DHIMA YA SILABI
– Silabi ni kipashio cha msingi ambacho kina dhima ya kifonotaktiki (kanuni ambayo inamruhusu mzungumzaji kutumia mfuatano unaokubalika na kumkataza mfuatano usiokubalika. Kwa mfano, katika Kiswahili hakuna silabi inayoundwa kwa mfuatano kappa. Hivyo basi, muundo wa silabi hutusaidia kujua mfuatano sahihi kulingana na lugha husika.
– Silabi inatumika kama mawanda ya kanuni za kifonolojia.
– Silabi ni kama muundo wa kipande sauti changamano. Silabi hupambanua/hudhibiti mfuatano wa sifa thabiti.
– Silabi ni kipashio ambacho hutumika kuunda vipashio vikubwa zaidi katika taaluma ya fonolojia kama vile toni, shada/mkazo. Pia inatumika kubainisha maana ya kifonolojia, kwa mfano, katika lugha ya Kiswahili tunaweka mkazo katika silabi ya pili kutoka mwisho wa neno.