Vielezi ni maneno yanayo fafanua vitenzi,vivumishi au vielezi vingine.huweza kuarifu kitendo kilichotendeka kilitendeka wapi,namana gana na hata mara ngapi. kuna aina tano ya vielezi ambavyo ni;
- Vielezi vya mahali
- Vielezi vya namna/jinsi
- Vielezi vya ala/kitumizi
- Vielezi vya wakati
- Vielezi vya idadi
(i) Vielezi vya mahali
Vielezi vya mahali ni maneno yanayofafanua kielezi kwa kueleza mahali ambapo kitenzi hicho
kilitendeka. Vielezi hivi huundwa kwa kutumia jina la mahali au kwa kuongeza kiambishi ‘-ni’
mwishoni mwa neno linaloashiria mahali. Kwa mfano;
Mwelusi alipelekwa gerezani.
Maimuna amefika Pumziko.
(ii) Vielezi vya namna/jinsi
Vielezi hivi hutoa taarifa ya ufafanuzi namna au jinsi kitenzi (tendo) kinavyofanyika. Vile vile,
vielezi hivi hujulisha kuwa kitenzi hicho kinatumika namna gani au jinsi gani.
kuna aina sita ya vielezi vya namna
(iii) Vielezi vya ala/kitumizi
Hutoa habari kuhusu kifaa, ala au mbinu iliyotumiwa kufanya kitendo Fulani katika muktadha
Fulani. Baadhi ya vielezi hivi ni kama vile kwa jembe, kwa meno, kwa moto, kwa kisu, kwa
miguu nk. Kwa mfano;
Kongowea alitembea kwa miguu hadi Kitale.
Dora limuuma Shangazi kwa meno.
(iv) Vielezi vya wakati
Hivi ni vielezi vinavyofafanua kitenzi kwa kujulisha wakati ambao tendo lilitendeka. Baadhi ya
vielezi vinaweza kuwa majina ya siku kama vile Jumatatu, Jumanne, Jumatano: Wiki, majina ya
miezi, mwaka, majira ya mwaka, nyakati za siku na matukio ya Kihistoria. Kwa mfano;
Mussa alitoroka jana.
Nyanyangu alifariki baada ya vita vya dunia.
(v) Vielezi vya idadi
Ni vielezi vinavyofafanuamara ngapi au kwa kiasi gani tendo limefanywa na kitendwa. Vielezi
vyenyewe vyaweza kuwa vya idadi kamili au ya jumla. Baadhi ya vielezi hivi ni kama vile;
moja, saba, chache, nyingi nk. Kwa mfano;
Wanamapinduzi walikamatwa mara nyingi katika Butangi.
Zena alimtembelea mara mbili.
Aina za Maneno |
Nomino-N |
Kiwakilishi-W |
Kivumishi – V |
Kitenzi-T, Ts au t |
Kiunganishi – U |
Kihusishi – H |
Kihisishi – I |