Zifuatazo ni aina za vihisishi

a) Vihisishi vya furaha

b) Vihishi vya masikitiko

c) Vihisishi vya kujuta

d) Vihisishi vya mshangao

e) Vihisishi vya huzuni

f)Vihisishi vya Kuapa

g) Vihisishi vya kuitikia

h) Vihisishi vya Kukataza

i) Vihisishi vya shukrani

j) Vihisishi vya Kufariji

k) Vihisishi vya kukataa

KihisishiMfano katika SentensiHisia
Lo!Lo! Maajabu ya Musa haya!mshangao
Salaale!, Masalaale!Salaale! Angalia watu wote hawa waliofika mahali hapa!mshangao
Kumbe!Nilidhani wewe ni rafiki yangu. Kumbe!mshangao
Po!Sijawahi kuona kijana mjeuri kama wewe. Po!hasira
Ng’o!Omba msamaha utakavyo, lakini unachoka bure. Ng’o!kiburi
Hata!Bwanake hakumwachia chochote! Hata!kusifia, kupuuza
Akh!, Aka!Mtoto mpumbavu huyu! Akh!hasira, kukashifu
Ah!Ah! Sikuyaamini macho yangu.mshangao
Ala!Ala! Umefika tayari!mshangao
Haha!Haha! Umenivunja mbavu, bwana!kicheko
Ehee!, Enhe!Enhe! Endelea, ninaipenda sana hadithi hiyo!kuitikia
Hmmm!Hmmm! Chakula kitamu hicho!kuitikia, kusifia
Ebo!Ebo! Tabia gani hiyo.kukashifu, hasira
Kefule!Kefule! Umenifedhehesha sana.hasira
Wee!Katamu alinegua kiuno na kucheza kwa madaha. Wee! Wavulana wakaduwaa.kusifia
La!, Hasha!La! Sitaki kusikiliza upuuzi wako tena.kukataa
Hoyeee!Wamama wote, hoyee! Hoyee!kushangilia
Huraa!Huraa! Tumeshinda.
Aina za Maneno
Nomino-N
Kiwakilishi-W
Kivumishi – V
Kitenzi-T, Ts au t
Kielezi-E
Kiunganishi – U
Kihusishi – H