Vitenzi ni maneno yanayosimamia kitendo. Kila kitenzi huwa na shina la kitenzi (sehemu ndogo
zaidi ya kitenzi ambayo ndiyo huwakilisha tendo hilo). Shina la kitenzi huambatanishwa na
viambishi ili kutoa maana iliyokusudiwa kama vile mtendaji, mtendewa, wakati kitendo
kinafanyika na pia kauli ya kitenzi hicho.

Kuna aina tano kuu za vitenzi nazo ni;

  1. Vitenzi Halisi
  2. Vitenzi Visaidizi
  3. Vitenzi Vikuu
  4. Vitenzi Vishirikishi
  5. Vitenzi Sambamba

Vitenzi Halisi (T)

kitenzi halisi ni ketenzi ambacho hutokea kikiwa peke katika sentensi na huchukua kiambishi cha wakati, hali na hata nafsi.Hivi ni vitenzi vinavyorejelea kitendo moja kwa moja. Vitenzi halisi vinapoambatanishwa na vitenzi vidogo katika sentensi, huitwa vitenzi vikuu.
k.m: soma, kula, sikiza
Waziri Mwasimba aliwasili jana kutoka ng’ambo.
Kawia atapikia wageni.
Funga mlango na dirisha.

Mama aliwapikia watoto chakula

Vitenzi vikuu (T)

Kitenzi kikuu ni kitenzi kinachobeba maana kuu katika sentensi na aghalabu hutokea kikiwa cha pili katika sentensi. Ni vyema kufahamu kuwa ikiwa sentensi itakua na vitenzi vitatu, cha tatu ndicho kitakua kitenzi kikuu. Kitenzi kikuu hutaja mambo matatu muhimu;

a) Tendo lenyewe k.m. mwanafunzi atakua amesafiri

b) Hali ya tendo k.m. Mwanafunzi alikua akisoma

c) kauli ya kitenzi k.m. Askari walikua wakipigana

Vitenzi Visaidizi ( Ts)
Vitenzi visaidizi ni vetenzi ambavyo husaidia vitenzi vikuu kutoa taarifa kamili na sahihi.Vitenzi hivi hutangulia vitenzi halisi (vitenzi vikuu) katika sentensi ili kuleta maana inayokusudiwa kulingana na wakati au hali. vitenzi hivi huweza kuonyesha wakati kitendo kikuu kinapofanyika, iwe ni wakati uliopita,uliopo au ujao
k.m: -kuwa, -ngali,
Jua lilikuwa limewaka sana.

Nyanya alikua akitusimulia hadithi
Bi Safina angali analala

Taarifa ingali inasomwa
Vitenzi Vishirikishi ( t)
Vitenzi vishirikishi ni vitenzi ambavyo hutumiwa kuonyesha ushirikiano au uhusiano baina ya nomino,kiwakilishi,kivumishi,au kielezi kingine.Vitenzi vishirikishi hutumika kuelezea hali iliyopo au mazingira. Kuna aina mbili za vitenzi vishirikishi:
a) Vitenzi Vishirikishi Vipungufu – vitenzi hivi havichukua viambishi vyovyote.
k.m: ni, si, yu,ndi,yu,li,u,wa,na,-ko, -mo,ya,ki,tu,m, n.k.
Kaka yako ni mjanja sana.
Huyo si mtoto wangu!
Paka wake yu hapa.

Yeye ni mkorofi

kiatu ki chini ya meza

sisi tu walimu
b) Vitenzi Vishirikishi Vikamilifu – ni vitenzi ambavyo huchukua viambishi vya nafsi au ngeli na viambishi vya wakati. Vitenzi hivi vinaweza kusimama peke yake au vinaweza kufuatiliwa na vitenzi vikuu.
k.m: ndiye, ndio, ndipo,kuwa,kutaka,kwenda,kujakwisha,ngali,kubidi,kupata.
Sangita ndiye mkurugenzi wa kampuni
Huku ndiko kulikoibiwa
Vitenzi sambamba

Vitenzi sambamba ni vitenzi viwili au zaidi vinavyotokea katika sentensi ili kuikamilisha kimaana.vitenzi hivi huwa sawa katika nafsi,wakati na hali.sentensi zenye vitenzi sambamba huundwa kwa vitenzi visaidizi na vitenzi vikuu.

Mfano katika sentensi;

wao walikwisha tambua alikua na nia mbaya

Yeye alilia akihuzunika

nyinyi mlikua hamjawahi kukariri mashairi

Aina za Maneno
Nomino-N
Kiwakilishi-W
Kivumishi – V
Kiunganishi – U
Kihusishi – H
Kihisishi – I