kiunganishi ni neno au kundi la maneno ambalo huunganisha vipashio vya lugha ili kuunda
kipashio kikubwa zaidi. Hali kadhalika ni maneno yanayounganisha maneno mengine.
Kiunganishi kinaweza kuunganisha neno na neno, kirai na kirai, kishazi na kishazi au sentensi na
sentensi.pasi na kuunganisha, viunganishi huweza kulinganisha au kuonyesha uhusiano wa
dhana mbili au zaidi.
Aina za viunganishi
Kama aina zingine za maneno, viunganishi vimegawika katika aina mbalimbali kulingana na matumizi yake. Aina hizi ni;
(i) Viunganishi vya kuonyesha umilikaji
Viunganishi hivi hutumika katika kuonyesha dhana ya umilikaji na ni vya aina mbili.

  • Viunganishi vya a-unganifu
    Viunganishi vya ngeli huundwa kwa kufungamanisha viambishi viwakilishi vya ngeli pamoja
    na kiungo –a. kama vile la, cha, vya nk. Kwa mfano;
    Kitabu cha Yusufu kimeibiwa.
    Gari la mwalimu ni jeusi.
  • Kiunganishi cha kwa
    Kiwakilishi hiki hutumiwa kuonyesha umilikaji wa mahali fulani, sababu, ala/kitumizi na
    mbinu. Kwa mfano,
    Nyumbani kwa savalanga kuliishi watoto wengi.
    (ii) Viunganishi vya Kujumuisha
    Mifano ni Na, Pia, Pamoja na, Licha ya, fauka ya, Zaidi ya, vilevile
  • (iii) Viunganishi vya Kuonyesha Tofauti
    Jambo kufanyika kinyume na matarajio. Baadhi ya viunganishi hivi ni kama; ingawa ,
    tofauti na, kinyume na, hata hivyo, ingawaje, japo, ijapokuwa, ilhali, ijapokuwa nk. Kwa
    mfano
    Baba aliondoka bila kusema lolote.
    Waliendelea kutenda dhambi minghairi ya kuhubiriwa kanisani jana.
    (iv) Viunganishi vya Kuonyesha sababu
    Mifano ya viunganishi hivi ni kama; Maadam, kwa vile, kwa maana, kwa kuwa, kwani kwa,
    minanjili ya nk. Kwa mfano
    Wanawake katika familia hiyo hawali maini maadam mama mkongwe alilaani maini katika
    familia hiyo.
    Madhali sote tuko hapa, tunaweza kuanzisha mkutano mapema.
    Hanna aliumizwa ili asikumbuke aliyoyaona.
    (v) Viunganishi vya Kuonyesha Matokeo
    Mifano ya viunganishi hivi ni kama; basi, kwa hivyo, hivyo basi na ndiposa. Kwa mfano
    Umekula ng’ombe mzima, hivyo basi huna budi kumalizia mkia.
    Gege alipenda kuimba sana, ndiposa akaitwa mkuki wa Almasi.
    (vi) Viunganishi vya kulinganisha
    Viunganishi hivi ni kama Katika, Miongoni mwa, Baadhi ya, Mojawapo ya
    Kwa mfano;
    Joni ni mfupi kuliko Mpapale.
    Wanafunzi hawafanyi kazi kulingana na maelezo ya mwalimu.
    (vii) Viunganishi vya Kuonyesha Kitu kufanyika badala ya kingine
    Mifano ya viunganishi hivi ni; Badala ya, kwa niaba ya na kwa.
    Kwa mfano
    Mapepo yalimchukua Shakawa badala ya bintiye.
    Mama Roga alitoa hotuba kwa niaba ya mumewe.
    (viii) Viunganishi vya Kuonyesha Kitendo kufanyika baada ya kingine
    Mifano ya viunganishi hivi ni; Kisha, halafu, basi
    Kwa mfano;
    Alichukua kisu halafu akatokomea gizani.
    (ix) Viunganishi vya Kuonyesha uwezekano
    Mifano ya viunganishi hivi ni; Labda, Pengine, Au, Ama, huenda
    Ama Anita au Katosha anaweza kuja.
    Sina pesa leo, labda uje kesho.
    (ix) Viunganishi vya Kuonyesha Masharti
    Mifano ya viunganishi hivi ni; Ikiwa, Almuradi, bora, Iwapo
    Kwa mfano
    Sitakuuliza bora tu usichelewe.
    Ikiwa huna jambo muhimu la kusema, nyamaza.
Aina za Maneno
Nomino-N
Kiwakilishi-W
Kivumishi – V
Kitenzi-T, Ts au t
Kielezi-E
Kihusishi – H
Kihisishi – I