Ala za matamshi ni viungo vya mwili wa binadamu vinavyotumiwa kutamkia sauti kwa njia moja au nyingine wakati wa kuongea.Kuna aina mbili kuu ya za ala za matamshi;
a) Ala tuli
b) Ala sogezi
Ala tuli/ ala pahala
Ni ala ambazo hazisogei wakati wa kutamka sauti. Ala hizi ni kama vile meno, ufizi, kaa kaa gumu, kaa kaa laini na koo/koromeo.
Ala sogezi
Ni ala ambazo husogea wakati wa kutamka sauti kama vile midomo na ulimi.
Majina ya Ala za matamshi
- midodmo ya juu
- Midomo ya chini
- Meno ya juu
- Meno ya chini
- Ufizi/masine
- Kaakaa gumu
- Kaakaa laini
- Chemba cha pua/ mkondo wa hewa pua
- Chemba cha Kinywa /Mkondo wa hewa kinywa
- Ulimi
- Ncha ya ulimi
- Bapa la uimi
- Shina la ulimi
- Kidaka tonge
- Nyuzi za sauti
- Koo/Umio wa hewa/Koromeo/ Zoloto