Alama ya hisi/ mshangao hutukima kwa njia zifuatazo:

  1. Alama hii hutumiwa kuamrisha 
  • Kachezeeni nje!
  • Kamau! Unafanya nini?
  1. Alama ya mshangao hutumiwa baada ya vihisishi
  • Masalaale! Pesa zangu zote zimeibwa.
  1. Alama hii hutumiwa baada ya sentensi iliyo mshangao
  • Gari langu limeibwa!
  1. Hutumiwa kusisitiza
  • Kesho msichelewe kuwasili shuleni!
  1. Alama hii hutumiwa kuonyesha kudharau/kubeza
  • Mwangalie! Kichwa kama jiwe.
  1. hutumiwa baada ya tanakali
  • Mate yalimdondoka ndo! Ndo! Ndo!