Alama ya Kinyota (*)

Alama ya kinyota (*) hutumiwa kwa njia zifuatazo:

1. Kinyota hutumiwa Kuonyesha neno ambalo litaelezewa zaidi chini ya ukrasa(foot note)

Alipopata nafasi ya kuingia shule ya upili ya Starehe*, mwanafunzi huyo alijawa na furaha tele.

*Starehe ni mojawapo ya shule zinazofanya vizuri zaidi barani Afrika

2. Kuficha herufi/silabi katika neno ili kupunguza ukali wa maneno yasiyo na nidhamu.

Rais aliwaita wananchi m**i ya kuku.

Aidha, alisema kwamba nyote ni wapu***vu.

3. Kinyota pia huonyesha kuwa neno limeendelezwa vibaya

    • *kitaabu

    4. Kinyota huonyesha sentensi haina mpangilio sahihi wa maneno 

      • *Kisu cha hiki ni nani?

      5. Kinyota huonyesha tanbihi (maelezo ya neno yanapatikana chini mwa ukurasa)

        • idhibati*

        6. Huonyesha sentensi ina makosa kisarufi

          • *Kuku hii ni ya nani?

          ALAMA ZA UAKIFISHA
          Alama za usemi(“”)
          Dukuduku (…)
          Koma/mkato/kipumuo( , )
          Ritifaa/kibainishi( ’ )
          Mshazari/mkwaju(/)
          Kistari kifupi( – )
          Kistari kirefu
          Mstari( ___  )
          Kikomo/kitone/nukta (.)
          Nusu/semi koloni/nukta na kituo (;)
          Vifungo/mabano/paradesi( )
          Herufi kubwa(H)
          Herufi ndogo (h)
          Koloni/ Nukta mbili ( : )
          Hisi/mshangao (!)
          Herufi nzito (h)
          Herufi za mlazo/italiki(h)
          Swali/Kiulizo

          Leave a Reply

          scroll to top