1. Kistari kifupi hutumiwa Kuunganisha maneno mawili
Askari-Jeshi watashika doria katika msitu wa shakahola.
Nawatuma kama wana-kondoo miongoni mwa mbwa-mwitu.
2. Kistari kifupi hutumiwa Kuonyesha hadi, au mpaka
Bei ya mafuta imepanda kutoka shilingi 160 – 180
Tutasoma Bibilia kitabu cha Marko 4: 3 – 9
3. Kama alama ya kupunguza au kutoa katika Hesabu
17 – 7 = 10
10 – 5 = 5
4. Kistari kifupi pia huonyesha neno ambalo halijakamilika litaendelezwa katika msitari ufuatao
Mwalimu alisafiri kutoka ulaya kuja kuwa-
tembelea wazazi wake baada ya miaka kumi.
5. Kuonyesha tarehe
Muhula wa tatu utaanza 28-08-2023.
Wanafunzi watafungua shule tarehe 04-02-2014