Alama ya Mlazo/Mshazari/mkwaju(/)

Alama ya Mshazari/mkwaju au mlazo hutumika kwa njia zifuatazo:

1. Alama ya mlazo hutoa dhana ya ‘au’

Mkutano huo utahutubiwa na Rais/Waziri Mkuu.

Wazungumzaji wengi wa Kiswahili wanatoka Kenyz/Tanzania.

2. Alama ya mlazo vilevile hutumiwa Kuonyesha neno au fungu la maneno lenye maana sawa.

Sheila amepewa cheo cha katibu/mwandishi.

Hawa ndio wanaotapatapa ovyo/wasio na mbele wala nyuma.

3. Alama ya mlazo hutumiwa Katika hesabu kuonyesha kugawanya au akisami.

5/7 ya siku za juma ni siku za kazi.

12 / 6 = 2

4. Alama ya mlazo hutumiwa Katika tarehe

Shule zilifunguliwa tarehe 08/01/2012

Kamati hiyo ilikubaliana kwamba, Mwokozi alizaliwa tarehe 25/12

ALAMA ZA UAKIFISHA
Alama za usemi(“”)
Dukuduku (…)
Koma/mkato/kipumuo( , )
Ritifaa/kibainishi( ’ )
Kistari kifupi( – )
Kistari kirefu
Mstari( ___  )
Kikomo/kitone/nukta (.)
Nusu/semi koloni/nukta na kituo (;)
Vifungo/mabano/paradesi( )
Herufi kubwa(H)
Herufi ndogo (h)
Koloni/ Nukta mbili ( : )
Hisi/mshangao (!)
Herufi nzito (h)
Herufi za mlazo/italiki(h)
Kinyota(*)
Swali/Kiulizo

Leave a Reply

scroll to top