1. Alama ya nukta mbili au koloni hutanguliza orodha:
Sherehe ya mama Maria ilihudhuriwa na watu wa wengi: wake kwa waume; wadogo kwa wakubwa; wazee kwa vijana.
Kuna aina kadhaa ya viwakilishi: Viwakilishi vya sifa, viwakilishi vya idadi, viwakilishi vya mahali n.k.
2. Koloni pia huelezea sababu au kuonyesha matokeo ya kitu.
Karanja alipoingia darasani alipigwa na butwaa: rafikiye Joshua alikuwa amezimia.
Koome alinipatia zawadi nzuri sana: nilirukaruka kwa furaha.
3. Koloni vilevile hutenga saa na madakika Kwa mfano:
Wanafunzi waliingia darasani 3:15.
Walifika uwanja ndege 6:45
4. Koloni hutumiwa pia Kunukuu ukurasa wa Bibilia
Mchungaji alisoma kitabu cha Luka 5:4-9
Katika kitabu chaYohana 8: 6-11, Bibilia inasema…
5. Koloni pia hutumiwaKuonyesha maneno ya msemaji katika tamthilia au mchezo wa kuigiza
Mwelusi: Unafikiria mimi ni mtu wa kuchezewa?
Sudi: (akitetemeka) Tafadhali naomba unisamehe.
6. Koloni pia huonyesha mada katika barua au kumbukumbu za mkutano
KUH: Ombi Lakuomba kazi yaUseremala
KUH: Barua ya tarehe 6/4/2009.KUM: 2/321/2020 Mbinu Mpya za Kunyamazisha Raia
7. Koloni hutumiwa Katika kumbukumbu za mkutano
KUM 2/321/2000: Mbinu mpya za kunyamazisha raia.
Ajenda 2: Kusomwa kwa kumbukumbu za mkutano uliotangulia.