Alama za usemi

Alama za usemi ( ‘ na “) hutumika kwa njia zifuatazo:

1. Kunukuu usemi halisi

“Ukitaka kufua dafu katika mtihani wa kitaifa,” mama akamwambia mwanawe, “lazima utie bidii masomoni na uwasikilize walimu wako.”

Alimtazama kwa macho makali kisha akamwuliza, “Unadhani nimechanganyikiwa kama wewe ambaye hukusoma?”

2. Kunukuu kichwa cha kazi ya sanaa k.v kitabu, wimbo, kipindi n.k

Rashid na Monica ni wahusika katika riwaya “Mwisho wa kosa”.

Reuben Kigame ndiye aliyeimba “Huniachi”.

3. Kuonyesha maneno yasiyo ya Kiswahili unapochanganya ndimi katika sentensi

Huyu ndiye mtu”Useless in this world”

Unaona “Cellphone” yake “computer” ni ya kisasa.

4. Kuonyesha maneno yanayowakilisha maana tofauti na maana yake ya kawaida au kinaya.

Maria alipoenda kwenye ‘shuleni’ alipachikwa mimba na ‘mwalimu’ wake.

Mwalimu ‘mkuu’ amewafukuza wanfunzi shuleni kwa madai ya kuchelewa.

Moto ulioteketeza shule hiyo ulitokana na kusudi la wanafunzi la ‘kumshtua’ mwalimu wao.

5. Kuonyesha herufi iliyoachwa nje au kufupisha maneno katika ushairi hasa kwa kusudi la kutosheleza idadi ya mizani

‘takufuata popote wendapo,

‘liapo ya mgambo, lazima kuna jambo

6. Katika maendelezo ya sauti ya ung’on’g’o (ng’)

Ng’ombe wa Ng’ang’a wanang’ang’ania nini?

King’ang’i anapenda kunung’unika ovyo ovyo.

ALAMA ZA UAKIFISHA
Alama za usemi(“”)
Dukuduku (…)
Koma/mkato/kipumuo( , )
Ritifaa/kibainishi( ’ )
Mshazari/mkwaju(/)
Kistari kifupi( – )
Kistari kirefu
Mstari( ___  )
Kikomo/kitone/nukta (.)
Nusu/semi koloni/nukta na kituo (;)
Vifungo/mabano/paradesi( )
Herufi kubwa(H)
Herufi ndogo (h)
Koloni/ Nukta mbili ( : )
Hisi/mshangao (!)
Herufi nzito (h)
Herufi za mlazo/italiki(h)
Kinyota(*)
Swali/Kiulizo

Leave a Reply

scroll to top