Changamoto za ufundishaji na usomaji wa ushairi

Utafiti unaonyesha kuwa kunachangamoto nyingi katika ufundishaji na usomaji wa ushairi. Changamoto hizo ni kama vile:

  1. Wanafunzi wengi wana mtazamo hasi kuwa ushairi ni dhana
    ngumu.
  2. Kuna baadhi ya walimu ambao pia wana mtazamo hasi kuhusu ushairi.
  3. Walimu kutojiandaa vyema katika somo hili.
  4. Upungufu wa vitabu teule vya ushairi katika shule zetu.
  5. Walimu kutowapa wanafunzi wao mazoezi ya kutosha ya ushairi.
  6. Walimu kutotambua mashairi yanayoendana na viwango vya wanafunzi, kilugha na kimaudhui.
  7. stilahi zinazotumiwa katika ushairi ni nyingi sana.

Namna ya kutatua changamoto za ufundishaji na usomaji wa ushairi

  1. Wanafunzi na baadhi ya walimu wabadilishe mtazamo wao kuhusu ushairi na waichukulie kama masomo mengine
  2.  Ufundishaji wa ushairi ulioratibiwa.
  3.  Kutoa ufafanuzi sahili kuhusu dhana ya ushairi na sifa zake.
  4. Mashairi mepesi na ya kuwavutia wanafunzi yateuliwe.
  5. Usomaji wa ushairi mara kwa mara ili kupevusha viwango.
  6. Wanafunzi washiriki utunzi wa mashairi mepesi.

  USHAIRI

1.        Historia ya Ushairi

2.        Changamoto za ufundishaji na usomaji wa uhairi

3.        Istilahi zinazotumika katika ushairi

4.        Sifa za mashairi ya kimapokeo

5.        Sifa za mashairi huru

6.        Kategoria kuu za mashairi

7.        Bahari za mashairi

8.        Uchambuzi wa mashairi

9.        Uhuru wakishairi

 

Leave a Reply

scroll to top