FONIMU KAMA ZILIVYOJADILIWA NA BLOOMFIELD.

 (I)                Fonimu sahili za msingi kama vile /p/, /k/, /z/ n.k

(II)             Fonimu changamani ambazo hutokana na muungano wa fonimu sahili ambazo hufanya kazi kama kitu kimoja kwa mfano, irabu unganifu.

(III)          Fonimu za upili ambazo hujitokeza kama muungano wa fonimu mbili au zaidi (kwa mujibu wa Bloomfield, vipambasauti vyote huangukia katika kundi hili).

Bloomfield anajadili pia sauti nyingine ambazo anaziita makundi maalumu ya fonimu, kwa mfano, anatofautisha fonimu zenye ukulele (vizuio, vimadende na vikwamizi) na zile zenye mlio wa kimuziki kama vile nazali, vitambaza, irabu n.k.)

Bloomfield anasema kuwa fonimu zinaweza kubainishwa kwa upambanuzi wa fonimu ujitokezao katika tabia yake ya kutofautisha maana na jinsi inavyoweza kuungana na vipashio vingine kuunda vipashio vikubwa zaidi. Naye anahimiza kuwa sifa za kifonetiki ni muhimu kwa sababu ndizo ziipazo fonimu utambulisho wake.

Kwa ujumla, Bloomfield anasema kuwa fonimu haiwezi kutazamwa katika upeke wake bali hutazamwa katika uamilifu wake katika lugha inayohusika. Kwa hakika dhana ya fonimu ya Bloomfield inashahabiana sana na dhana ya fonimu ya Trubetzkoy.

hati miliki zimehifadhiwa

Leave a Reply

scroll to top