Herufi kubwa Herufi kubwa hutumika kwa jinsi tatu zifuatazo:

  1. Hutumiwa mwanzoni mwa sentensi.
  2. Mwanzoni mwa mshororo katika beti za shairi au nyimbo.
  3. Kutaja herufi za mwanzoni za nomino za nomino za pekee. Kuna mifano mingi kama vile:

a) Jina la mtu: Maria, Yohana,Peter n.k.

b) Neno linalotaja cheo mahususi: Mhandisi , Mkurugenzi Mkuu, n.k.

c) Neno kuu lililomo katika anwani ya kitabu, makala, gazeti, insha n.k.

d) Siku za juma na miezi ya mwaka: kama vile Jumapili, Ijumaa, Aprili, Disemba, n.k.

e) Majina ya nchi: Uhispania, Marekani, Japani,Tanzania,Uganda n.k.

f) Majina ya lugha: Kiswahili,Kiingereza,’ Kizulu, Kijerumani, Kijaluo, (Dholuo) n.k.

g) Majina ya dini: Kibudha,Kikristo, Kiislamu, n.k.

h) Majina ya mitaa na barabara: Barabara ya Uburu, Mtaa wa Buruburu, Njia kuu ‘ya Maendeleo.

i) Matumizi maalumu tofauti na yale ya ujumla. Mfano: Nitatembelea Chuo Kikuu cha Nairobi.

j) kuandika anwani

  • S.L.P 1000, Bumala.

k.) Mwanzoni mwa usemi halisi

  • “Twendeni zetu,” akatwambia. 

l) baada ya kiulizi (?) na hisi (!) 

  • Lo! Ulienda? Hebu niambie yaliyojiri.                                                                                              

m) Mwanzoni mwa nomino za pekee

  • Musa

n) Ufupisho wa maneno 

  • C.C.M (Chama cha Mapinduzi)

o) Kuandika  sifa inayotokana na jina la pekee

  • Kiganda, Kikristu.

p) Uandishi wa onyo au tahadhari