Herufi za mlazo au italiki hutumiwa kwa njia zifuatazo:

  1. Herufi za mlazo huonyesha aina ya kiambishi au mofimu
  • Ki-li-cho-ib-w-a (kirejeshi).
  1. Herufi za mlazo hutumiwa kusisitiza
  • Jibu maswali mawili.
  1. Herufi za mlazo hutumiwa pia kuonyesha jina la kitabu
  • Nyota ya Rehema
  1. Herufi za mlazo hutumiwa kuonyesha maneno ya kigeni
  • Napenda mukimo.
  1. Herufi za mlazo hutumiwa kuonyesha maelezo ya vitendo vya mhusika katika mazungumzo, mahojiano na tamthilia
  • AMINA: (Akiinuka) Mama ameenda kwa Farashuu.