HISTORIA YA TAFSIRI AFRIKA MASHARIKI

 Taaluma hii ya tafsiri ina historia ndefu hapa dunia tangu kale, lakini kwa hapa  Afrika mashariki kwa ujumla historia hii ya tafsiri haina historia ndefu kwani inaanzia karne ya 19 ambapo wamisionari walitafsiri vitabu mbalimbali vya kikristo ikiwemo biblia kutoka lugha ya kiingereza kwenda Kiswahili na lugha nyingine za makabila makubwa nchini Kenya

Na hata wakati wa utawala wa kikoloni hasa waingereza walitafsiri maandiko mbalimbali ya taaluma na fasihi ya Ulaya kwa lugha ya Kiswahili Na hata baada ya uhuru wapo wazalendo waliofanya juhudi za kutafsiri vitabu mbalimbali kwa lugha ya Kiswahili mfano mzuri ni Rais wa kwanza wa Tanzania Mwalimu Julius K. Nyerere ambaye alitafsiri vitabu viwili vya mwandishi mashuhuri wa tamthiliya wa Uingereza William Shakespeare ambavyo ni: Juliasi Kaizari [1963] na Mabepari wa Venisi[1969] {Tazama pia Mwansoko na wenzake 2006 : 5}

Mfano wa tafsiri ambazo zimetafsiriwa kwa lugha ya Kiswahili ni pamoja na ya,Ayi Kwei Armah, Wema Hawajazaliwa ambayo imetafsiriwa na Abdilatif Abdalla, House boy ya Ferdinand Oyono iliyotafsiriwa na Raphael Khasao na Nathan Mwele. Juliasi Kaizari na Mabepari wa Venisiza zaWilliam Shakespeare zilizotafsiriwa na Julius K. Nyerere, Hekaya za Abunuwasi, Kimetafsiriwa na Interterritorial Language Committee, East Africa, Alfu Lela Ulela: Kimetafsiriwa na Sir Richard Burton na Mashimo ya Mfalme Suleiman kilichotafsiriwa na Sir Rider Haggard, Takadini,kimetafsiriwa na Mathews Bookstore and Stationers, Nitaolewa Nikipenda ambacho kimetafsiriwa na Crement M. Kabugi. vitabu vingine vilivyotafsiriwa ni kama vile; Orodha, Barua Ndefu Kama Hii n.k.

Mpaka sasa wataalamu mbalimbali wamekuwa wakiendelea kutafsiri maandiko mbalimbali kama vile mikataba na ripoti mbalimbali za kimataifa, sheria ambazo mwanzo zilikuwa zikiandikwa kwa lugha ya kiingereza, vitabu vya kiada na ziada, kazi za kifasihi, n.k

MAREJEO

Cartford [1995] A linguistic Theory Translation

Mwansoko, H.J.M na wenzake [2006] Kitangulizi cha Tafsiri, Nadharia na

Mbinu.TUKI.Dar-es-salaam

Newmark, P [1982] Approaches to Translation, Oxford, Pergamon Press

Newmark, P [1988] A Text book of Translation, London, Prentice Hall.

Oxford University Press Dar-es-salaam

Semzaba, E [2006] Ngoswe, Penzi Kitovu cha Uzembe. The General Booksellers LTD.

D.S.M

TUKI [2002] Kamusi ya Kiswahili Sanifu. TUKI, Dar-es-salaam

TUKI [1985] Kiswahili, Jarida la Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili.

www.bakita.org.tz retrieved on Monday 04th July 2018

www.jim-mission.org.uk retrieved on Monday, 04th July 2018

www.ajol.inf retrieved on Monday, 04th July 2018

Vitabu vilivyotafsiriwa ambavyo vimetumika kama marejeo

Ayi Kwei Armah, Wema Hawajazaliwa, kimetafsiriwa na Abdilatif Abdalla

Ferdinand Oyono: House boy, Kimetafsiriwa na Raphael Khasao na Nathan Mwele.

William Shakespeare: Juliasi Kaizari: Kimetafsiria na Julius K. Nyerere

Mabepari wa Venisi: Kimetafsiriwa na Julius K. Nyerere

Hekaya za Abunuwasi: Kimetafsiriwa na Interterritorial Language Committee, East Africa

Alfu Lela Ulela: Kimetafsiriwa na Sir Richard Burton

Sir Rider Haggard: Mashimo ya Mfalme Suleiman


hati miliki zimehifadhiwa

Leave a Reply

scroll to top