Historia ya Ushairi

 

Ni vigumu sana kuelezea wakati ushairi wa Kiswahili ulipoanza.
Wapo baadhi ya watu wanoamini kuwa ushairi ulikuwepo tangu Karne Pili. Wapo pia
wanaoamini kuwa ushairi ulianza mtu alipobuni lugha. Lakini inaaminika kuwa,
chimbuko la Ushairi wa Kiswahili ni kutokana na nyimbo zilizotumia nyakati za
sherehe mbalimbali kama harusi, jando, nyakati za kufanya kazi, nk. Nyimbo hizo
hazikufuata arudhi tunazozifahamu za ushairi wa kisasa, ila baadaye ziwekwa
vina na hatimaye kuwiana hata kwa mizani.

Zipo nadharia nyingi
zinazoelezea kuhusu historia ya Ushairi tangu wakati huo hadi sasa. Ipo
nadharia inayodai kuwa Chimbuko la ushairi wa Kiswahili ulitokana na ujio wa
Waarabu. Nadharia nyingine inasema kuwa Chimbuko la Ushairi wa Kiswahili ni kwa
jamii ya waswahili wenyewe. Lakini ni dhahiri kwamba chimbuko la Ushairi wa
Kiswahili ni kutoka kwa Waswahili wenyewe. Waswahili wana utamaduni wao ambao
ulikuwepo hata kabla ya ujio wa Waarabu. Na waliutumia Ushairi huo katika
shughuli mbalimbali za kijamii.

Historia ya Ushairi wa Kiswahili ni ndefu mno ila wataalamu
wameumegawanya muda huo wote kwa vipindi vinne.

Kipindi
Cha Kwanza (Urasimi Mkongwe)

Kipindi hiki ni wakati wa mashairi yaliyotungwa kabla ya karne
ya kumi na nane. Katika kipindi hiki, mashairi yalikuwa kakitungwa ila hayakuwa
na utaratibu wa vina, vina, mizani na beti kama ilivyo katika mashairi ya
kisasa. Mashairi ya siku hizo yalikuwa kama nyimbo tu na yalikuwa na
mishororo mirefu. Mashairi hayo yalibadilika kimaudhui, jamii nazo zikipambana kutunga
kwa maudhui mbalimbali.

Mashairi ya myakazi hizo, yalipashwa tu wakati wa sherehe
mbalimbali kwa kuwa ustaarabu wa kuandika ulikuwa bado kwa Waswahili.
Mabadiliko mengi yalifanyika Waarabu walipofika pwani ya Afrika Mashariki.
Waarabu walikuwa na mashairi yao yaliyokuwa na vina beti, mizani na maudhui ya
kidini (dini ya Kiislamu). Tangu wakati huo, mashairi yakfuata mkondo huo.
Waswahili wakafunzwa hati ya Kiarabu ili kusoma Kurani Tukufu.

Hizo ndizo nyakati ambazo inadhaniwa kuwa shairi la kwanza liliandikwa
kwa kufuata kanuni za Ushairi. Japo kulikuwa na mashairi mengine hapo awali,
Utenzi wa Tambuka (Chuo cha Herekali) unadaiwa kuwa wa kwanza kuandikwa kwa
kufuata kanuni za Ushairi. Utenzi huo ulitungwa na Mwengo Bin Athumani
(1728-1840) na ulihusu maisha ya Sultani wa Pate ‘Fumo Laiti Nabhani’.

Tungo nyingine za wakati huo:

1.                
Utenzi wa Hamziya (1749) – Sayyid Abdarus

2.                
Utenzi wa Mwanakupona (1859)

3.                
Utenzi wa Al-Inkishafi (1813) – Sayyid Abdallah A. Nassir

4.                
Utenzi wa Rasi-al-Ghuli

5.                
Utenzi wa Shufaka

6.                
Tungo za Muyaka bin Haji Al Ghassany (1776-1840)

7.                
Tungo za Ali Kofi

8.                
Tungo za Bwana Mataka

Kipindi
Cha Pili (Kipindi cha Utasa)

Kipindi hiki ni miaka kati ya 1885 na 1945. Huu ulikuwa wakati
wa utasa. Huu ulikuwa wakati wa ukoloni. Mashairi mengi yaliyotungwa katika
kipindi hiki yalihusu utumwa na kujikomboa kutoka kwa wakoloni.

Baadhi ya waliotunga katika kipindi hiki ni kama:

1.                
Utenzi wa Vita vya Majimaji

2.                
Utenzi wa Abdirahman na Sufiyani (1939-1945) – Hemed Abdalla

Kipindi
Cha Tatu (Urasmi Mpya)

Kipindi hiki kilikuwa kati ya 1945 na 1960. Washairi walitunga
kwa kufuata kanuni za ushairi. Wengi wa watunzi hao walitunga mashairi ya
tarbia ingawa wengine kama Shaana Roberts walitunga aina tofauti ya mashairi.
Kipindi hiki kilikuwa cha Wanajadi au Wanamapokeo walishindania ufundi. Ilikuwa ni
lazima kila mtunzi kutumia arudhi za ushairi ili kuonyesha kuwa, alikuwa bora
kuliko mwengine. Shairi ambalo halikufuata kanuni hizo, halikuaminika kama
shairi kamili na liliitwa guni. Waliamini kuwa shairi ni lazima liwe urari wa
vina na ulingasnifu wa mizani.

Tamasha mbalimbali ziliandaliwa na watunzi kuwasilisha tungo zao
na kufanyiwa uamuzi na watunzi waliobobea wakajulikana kama mashekhe.
Waliofaulu walivikwa umalenga nawaliopungukiwa katika arudhi yoyote kubezwa na
kuvikwa guni.

Watunzi waliosifika sana wakati huo walikuwa kama:

1.                
Mwengo Bin Athumani

2.                
Muyaka bin Haji

3.                
Mwalimu Sikujua

4.                
Said Karama

5.                
Amri Abedi

6.                
Ahmad Nassir

7.                
Shaaban Robert

Umaarufu wa washairi wa kipindi hiki ulidhihirika wakati wa
tamasha mbalimbali na sherehe kama za arusi, mazishi na burudani. Tamasha hizo
zilisaidia kunoa na kuboresha vipawa vyao.

Kipindi
Cha Tatu (Urasmi Mpya)

Katika kipindi hiki, kulizuka wasomi wenye ujuzi katika Fasihi
ya Kiswahili. Wasomi hao walijiita Wanamapinduzi. Walijitokeza na aina ya mashairi
yanayojulikana kama Mashairi Huru na kudai kuwa yanakubalika katika kama
mashairi mengineyo.

Wanamapinduzi hao walisitiza kuwa mashairi ya arudhi yalimfunga
sana mshairi kupasha ujumbe wake vizuri. Walidai kuwa mshairi hakuweza
kujieleza vizuri kwa kuwa ilikuwa ni lazima ajibiidishe kwanza kutafuta maneno
yatakayolinganisha vina na kutosheleza mizani. Waliamini kuwa mtunzi ana uhuru
wa kutunga aina za mashairi wazipendazo bora tu wapashe ujumbe kwa hadhira.
Washairi hao walitunga mashairi bila kujali arudhi za ushairi, jambo ambalo
lilizua mgogoro katika
Ushairi wa Kiswahili.

Baadhi ya watunzi hao ni kama:

1.                
Euphase Kezilahabi

2.                
Mugyabuso Mulokozi

3.                
Ebrahim Hussein

4.                
Alamin Mazrui

5.                
Kithaka wa Mberia

6.                
Kulikoyela Kahigi

 

    USHAIRI

1.        

Historia ya Ushairi

2.        

Changamoto za ufundishaji na usomaji wa uhairi

3.        

Istilahi zinazotumika katika ushairi

4.        

Sifa za mashairi ya kimapokeo

5.        

Sifa za mashairi huru

6.        

Kategoria kuu za mashairi

7.        

Bahari za mashairi

8.        

Uchambuzi wa mashairi

9.        

Uhuru wakishairi

hati miliki zimehifadhiwa

Leave a Reply

scroll to top