Kirejeshi ‘amba-’ na kirejeshi ‘o’ hutumiwa kurudisha fikra zetu kwenye kitu kilichotajwa hapo awalli. Tanbihi: Ni makosa ya kisarufi kuchanganya kirejeshi ‘amba-’ na ‘o’ katika sentensi moja.

Matumizi ya kirejeshi ‘amba-’ katika sentensi:

(a) Kiatu ambacho kilipotea jana kimepatikana.

(b) Mwanafunzi ambaye hakuhudhuria masomo jana amefika shuleni

(c) Maji ambayo yalimwagika ni ya mvua.

(d) Sara ambaye ni bibiye Hassan amepewa talaka.

Matumizi ya kirejeshi ‘o’ katika sentensi

(a) Kiti kilichonunuliwa jana kimevunjika.

(b) Mkulima afanyaye kazi kwa bidii huvuna vizuri.

(c) Maji yaliyomwagika ni ya mvua.

(d) Shamba lililolimwa jana limetoa mazao bora.

Tanbihi:

  1. Ukiambiwa uondoe kirejeshi ‘amba-‘ katika sentensi unastahili kutumia kirejeshi ‘o’. Kwa upande mwingine, ukiambiwa uondoe kirejeshi ‘o’ katika sentensi, unastahili kutumia kirejeshi ‘amba-‘.
  2. Kirejeshi ‘o’ kikitumiwa kama kiambishi tamati huwa na maana ya hali ya mazoea.
  3. Kirejeshi ‘o’ hujitokeza kama ‘ye’ katika ngeli yaA-WA, umoja,