Kiima ni sehemu_ inayozungumziwa katika sentensi. Sehemu hii inaweza kuundwa na nomino au kiwakilishi cha nomino, na pengine pamoja na kivumishi, au kielezi lakini bila kitenzi. Aidha, tunaweza kueleza kiima kama neno au kifungu cha maneno katika sentensi ambacho hutangulia kitenzi na aghalabu huonyesha mtenda. Mifano: (a) Yeye ni rafiki yangu.
(b) wanafunzi na walimu wanasoma.
(c) Kondoo mkubwa sana amechinjwa.
(d) Maria anapenda kusoma.
KUMBUKA: Kiima kinaweza kuwa kiambishi kinachosimamia nomino. Mifano: Tunaimba.,Anasoma.
Kiarifu ni sehemu inayotoa taarifa kuhusu kiima. Sehemu hii huanza kwa kitenzi na pengine huwa na kitenzi pamoja na kivumishi, kitendewa au kielezi. Mifano: baba anasoma vizuri, mwanafunzi atakimbia mara sita.