Alama hii ya uakifishaji hutumiwa kama ifuatavyo;

  1. mwishoni mwa sentensi kuonyesha kuwa sentensi imekamilika kwa mfano; maria atasoma kwa bidii. – Katibu mkuu atasoma taarifa ya waziri wa kilimo – Nasieku ameenda sokoni kununua matunda
  2. Kuonyesha ufupisho wa maneno kwa mfano: prof., Dakt., Bi., Bw. – Bw. Thuo ni chifu wa kata hii ya Pondamali – Dkt. Mugo hutibu magonjwa sugu
  3. Kutenga fedha – shillingi na senti. kwa mfano: 6.50 Aminunua kitabu shillingi sita na senti hamsini 6.50 Amenunua nyaya za shillingi thelathini na senti hamsini 30.50
  4. Katika uandishi wa tarakimu kuonyesha saa na tarehe. Mifano: a) Kutenganisha saa na dakika Sasa ni saa 7:20 Asubuhi b) Kutenganisha tarehe; siku, mwezi na mwaka 13.07.2023 c) kuonyesha kutokamilika kwa tarakimu; Alipata alama 30.5 kwa mia katika somo la kiswahili
ALAMA ZA UAKIFISHA
Alama za usemi(“”)
Dukuduku (…)
Koma/mkato/kipumuo( , )
Ritifaa/kibainishi( ’ )
Mshazari/mkwaju(/)
Kistari kifupi( – )
Kistari kirefu
Mstari( ___  )
Nusu/semi koloni/nukta na kituo (;)
Vifungo/mabano/paradesi( )
Herufi kubwa(H)
Herufi ndogo (h)
Koloni/ Nukta mbili ( : )
Hisi/mshangao (!)
Herufi nzito (h)
Herufi za mlazo/italiki(h)
Kinyota(*)
Swali/Kiulizo