Kishazi ni mpangilio wa maneno wenye kiima (nomino)na kiarifa(kitenzi) au kiarifa pekee ambayo huwa sehemu ya sentensi kuu.
Kishazi ni kundi la maneno lenye kiima na kiarifu likiwa ndani ya sentensi kuu.
mifano;
i) Wanafunzi wanasoma darasani.
ii) Tutamwandikia mwenyekiti barua.
iii) Tuliwalisha watoto vyakula vingi.
kishazi ni tungo inayotawaliwa na kitenzi. Kitenzi hicho kinaweza kuwa kinajitosheleza kimaana au kisijitoesheleze kimaana. Kile kinachojitosheleza kimaana – basi hutoa taarifa kamili wakati kile ambacho hakijitoshelezi kimaana hakitoi taarifa kamili. Hivyo basi ni lazima kiambatane na kishazi (kitenzi) kingine ndipo taarifa yake ikamilike.
kwa ufupi tunaweza sema kuwa kishazi ni aina ya utungo ambao huwa na kitenzi ndani yake, kitenzi hicho kinaweza kikawa kinakamilisha maana au kisiwe kinajikamilisha kimaana. Kitenzi ambacho huwa kinakamilisha maana huwa ni kitenzi kikuu (T), na kile kisichokuwa kinatoa taarifa kamili huwa ni kitenzi kisaidizi (TS). Kwa mujibu huo tunapata aina mbili ya vishazi yaani kishazi huru na kishazi tegemezi.