Kishazi huru (K/Hr)
Kishazi huru ni kifungu cha maneno katika sentensi ambacho hutoa maana kamili. Kishazi huwa na tabia ya kutoa taarifa ambayo huwa ni kamili katika tungo, hubeba kitenzi kikuu au kishirikishi ndani yake. Kishazi hiki huwa hakihitaji maelezo ya ziada ili kukamilisha maana au taarifa kusudiwa na pia huweza kujitegemea kama sentensi kamili na huwa na muundo wa kiima na kiarifu.
Mfano; Tazama jedwali lifuatalo:
Kiima | Kiarifa |
Mama | anapika chakula |
mwalimu | anamfahamu |
chifu | amempiga vibaya |