Kishazi tegemezi (K/ Tg)
Aina hii ya kishazi huwa hakitoi taarifa iliyokamili badala yake hutegemea kishazi huru ili kukamilisha taarifa iliyokusudiwa na msemaji. Kishazi hiki hutawaliwa na kitenzi kisaidizi. Kishazi tegemezi kwa upekee wake hakiwezi kutoa taarifa iliyokusudiwa. Vishazi tegemezi hushuka hadhi na kuwa na hadhi ya kikundi cha maneno (kirai).
Mfano; Mtoto unayemjua
Mwanafunzi anayesoma
Mahali alipoingia
Mama alipomchapa
Kaka aliporudi
Vishazi hivyo hapo juu havitoi taarifa iliyokamili ila tunapoviweka pamoja na vishazi huru taarifa iliyokusudiwa hukamilika. Tazama hapa chini:-
Mfano; Mtoto unayemjua ameondoka
Mwanafunzi anayesoma atafaulu
Mahali alipoingia ni pachafu
Mama alipomchapa aliondoka
Kaka aliporudi alinifurahisha