koma/Kipumuo/Mkato/Kituo

Kuma hutumiwa katika maandishi kama ifuatavyo;

  1. Kuonyesha mtuo katika usomaji. Kwa mfano: Ikiwa utapita mtihani wako vizuri, nitakununulia zawadi.
  2. Katika uandishi wa anwani ya barua. Kwa mfano: Shule ya upili ya Goseta, S.L.P 22021, Kitale.
  3. Kutenganisha maneno kwenye orodha. Kwa mfano : Tulipofika sokoni tulinunua mahindi, mchele, mboga, matunda na unga wa ngano.
  4. Hutumiwa baada ya usemi halisi. Mfano katika sentensi: “Usipotoka hapo utashtakiwa,” Askari alisema.
  5. Hutumiwa pia baada ya mamneno kama ndio, la, asante, je, na kadhalika. Mfano katika sentensi: Ndio, nitakuandikia barua leo jioni. La, sitasoma hadithi hiyo ya kuhuzunisha.
  6. Hutumiwa baada ya kutaja jina la mtu anayepewa habari. Mfano katika sentensi: “Baba, naomba unisamehe kwa kukukosea,”Nilimsihi babangu. “Wanangu, mpende mungu zaidi ya yote,” Kasisi alihubiri
ALAMA ZA UAKIFISHA
Alama za usemi(“”)
Dukuduku (…)
Ritifaa/kibainishi( ’ )
Mshazari/mkwaju(/)
Kistari kifupi( – )
Kistari kirefu
Mstari( ___  )
Kikomo/kitone/nukta (.)
Nusu/semi koloni/nukta na kituo (;)
Vifungo/mabano/paradesi( )
Herufi kubwa(H)
Herufi ndogo (h)
Koloni/ Nukta mbili ( : )
Hisi/mshangao (!)
Herufi nzito (h)
Herufi za mlazo/italiki(h)
Kinyota(*)
Swali/Kiulizo

Leave a Reply

scroll to top