Konsontanti zinapotamkwa, hewa huzuiliwa katika ala za matamshi.Konsonanti za kiswahili huanishwa kwa kutumia vigezo vifuatavyo:

  1. mahali pa kutamkia( ala inayotumika katika kutamka konsonanti husika/mahali hewa inapozuiliwa inapotoka mapafuni)
  2. mtetemeko katika nyuzi za sauti/glota ( ughuna au usoghuna wa sauti)
  3. Jinsi ya kutamka sauti/ namna hewa inavyo zuiliwa

A] Mahali pa kutamkia

kwa kurejelea kigezo hiki kuna sauti zifuatazo:

  • sauti za midomo

Hizi ni sauti ambazo wakati wa matamshi midomo (lips) hutumika.Vitamkwa hivyo ni kama vile /p/, /b/, /m/ na /w/ 

  • Sauti za midomo na meno

Ni sauti ambazo zinahusisha midomo na meno wakati wa matamshi, sauti hizo ni mbili tu nazo ni /f/ na /v/.

  • Sauti za Ufizi

Hizi ni sauti ambazo hutamkiwa kwa ufizi. sauti hizi ni /t/, /d/, /n/, /s/, /s/, /r/, na /l/

  • Sauti za Kaa kaa Gumu

Ni sauti ambazo hutamkiwa katika kaa kaa gumu nazo ni  sauti /ch/, /j/, /ny/, /sh/, /y/

  • Sauti za meno

Ni sauti ambazo zinapotamkwa meno hutumika, sauti hizi ni /th/, na /dh/

  • sauti za kaa kaa laini

Ni sauti ambazo hutamkiwa katika kaa kaa laini sauti hizo ni /k/,/g/, /ng’/, /gh/

  • Sauti za Koromeo

Ni sauti ambayo hutamkiwa katika koromeo. sauti hii ni moja tu nayo ni /h/

b] Mtetemeko katika nyuzi za sauti

katika kigezo hiki huwa kuna aina mbili kuu ya sauti nazo ni:

       i) Sauti zisizo ghuna/sighuna/sauti hafifu

Hizi ni sauti zinapotamkwa nyuzi za sauti huwa hazitikisiki. sauti hizi ni kama vile: /p/, /t/, /k/, /f/, /th/, /s/, /sh/,/h/ na /ch/

       ii)Sauti ghuna

Hizi ni sauti zinapotamkwa hutikisa nyuzi za sauti. Sauri hizi ni kama vile: /b/,/d/,/j/,/g/,/v/,/dh/,/z/,/gh/,/m/,/n/,/ny/,/ng/,/l/,/r/,/w/ na /y/

C] Jinsi ya kutamka sauti

Hiki ndicho kigezo cha tatu na cha mwisho katika uanishaji wa konsonanti, kutokana na kigezo hiki tunapata sauti zifuatazo:

  • Vipasuo/Vizuio

Ni konsonanti ambazo wakati wa kutamkwa hewa husukumwa, huzuiliwa kabisa na kuachiliwa kwa ghafla na mpasuko mdogo kutokea. sauri hizo ni kama vile /p/,/b/,/t/,/d/,/k/ na /g/

  • Vikwamizo/Vikwaruzo

Hizi ni konsonanti ambazo wakati wa kutamkwa hewa kutoka mapafuni huptishwa taratibu au polepole.Ala za kutamkia nazo hukaribiana sana,hewa hii inapopita, hukwamizwa na kuoa mlio kama kwaruzo. Sauti hizi /f/, /v/,/th/,/s/,/t/,/sh/,/gh/ na /h/

  • Vipasuo kwamizo/kwaruzo

Ni konsonanti ambayo wakati wa kutamkwa hewa husukumwa nje kwa nguvu, huzuiliwa kabisa halafu mwanya mdogo huachwa hewa ipite kwa kukwamizwa. sauti hii ni moja tu nayo ni /ch/

  • Nazali/Ving’ong’o

Hizi ni konsonanti ambazo wakati wa kutamkwa kuna kiasi cha hewa huachiliwa na kupitia puani. Sauri hizi ni  /m/, /n/, /ny/ na /ng’/

  • Kitambaza

Hii ni konsonanti ambayo wakati wa kutamkwa hewa husukumwa kwa nguvu na  kuzuiliwa na kisha kuachiliwa ipite taratibu pembeni mwa ufizi na ncha ya ulimi.katika lugha ya kiswahili kitambaza ni kimoja nacho ni /l/ 

  • Kimadende

Kimadende ni konsonanti ambayo wakati wa kutamkwa hewa husukumwa, kuzuiliwa na kuachiliwa na kusababisha ncha ya ulimi kupigapiga ufizi mfululizo. Sauti hii ni /r/ katika kiswahili

  • Nusu irabu/Viyeyusho

Hizi ni konsonanti ambazo wakati wa kutamkwa hewa hupitishwa katikati ya ala kwa ulaini kama katika utamkaji wa irabu. sauri hizi ni mbili nazo ni /w/ na /y/

        Zoezi 

  1. Tambua kikwamizo cha kaakaa laini na kiyeyusho cha midomo.
  2. Tambua konsonanti ambazo si za orodha hii na ueleze kwa nini: /m/, /n/, /ny/,/ng’/, /f/, /b/
  3. Tofautisha konsonanti /p/ na /dh/.
  4. Taja konsonanti mbilimbili ambazo hujulikana kama:
    1. viyeyusho
    2. vikwaruzo

Jedwali Uainishaji wa Konsonanti 

KonsonantiAINA/Jinsi ya kutamkaMahali pa kutamkiaAthari kwa nyuzi za sauti
/p/KipasaoMidomosighuna
/b/KipasaoMidomoghuna
/k/KipasaoKaa kaa lainisighuna
/j/KipasaoKaa kaa gumughuna
/g/Kipasaokaa kaa lainighuna
/d/Kipasaoufizighuna
/m/Nazalimidomoghuna
/n/Nazaliufizighuna
/ng’/Nazalikaa kaa lainighuna
/ny/Nazalikaa kaa gumughuna
/dh/kikwamizomenoghuna
/f/kikwamizomeno na midomosighuna
/gh/kikwamizokaa kaa lainighuna
/h/kikwamizokoromeosighuna
/s/kikwamizoufizisighuna
/ch/Kipasuo kwamizokaa kaa gumusighuna
/l/kitambazaufizighuna
/r/kimadendeufizighuna
/sh/kikwamizokaa kaa gumusighuna
/th/kikwamizomenosighuna
/v/kikwamizomidomo na menoghuna
/z/kikwamizoufizighuna
/t/Kipasuoufizisighuna
/y/Kiyeyusho/nusu irabukaa kaa gumughuna
wKiyeyusho/nusu irabumidomoghuna

     Matamshi/

                        MAHALI  AINA MIDOMOMDOMOMENOMENOUFIZIKAAKAAGUMUKAAKAALAINIKOROMEO
VIPASUO            (H)                           (GH)pbtd
kg
VIPASUO         (GH)KWAMIZO          (H)chj
NAZALI            (GH)(VING’ONG’O) mnnyng’
VIKWAMIZO      (H)(VIKWARUZO)(GH)fvthdhszshghh
KITAMBAZA   l
KIMADENDE   r
NUSU IRABU VIYEYUSHO    wy