Lugha ni mfumo wa sauti za nasibu zenye maana na zilizokubaliwa na jamii ya watu fulani ili zitumike katika kuleta mawasiliano.
Lugha ni mfumo wa sauti za nasibu kwa sababu zilitokea kama bahati tu kwa binadamu. kwa hivyo hamna uhusiano baina ya neno linalotumiwa na kitu ambacho neno hilo liniwakilisha kwa mfano neno neno kiti halina uhusiano wowote na kifaa chenyewe linatumika tu kwa sababu ni makubaliano tu baina ya watumizi wa lugha hii kwa hivyo matumizi ya neno hili ni wa kinasibu tu.
Lugha ni chombo cha mawasiliano baina ya binadamu. Mawasiliano kwa kawaida hufafanuliwa kama “kupashana au kubadilishana mawazo, maoni, au habari kwa maneno, maandishi au ishara.
wataalamu mbalimbali wamefasiri lugha kama ifuatavyo;
Weber(1985). Anasema kuwa lugha ni mfumo wa mawasiliano ya mwanadamu ambao hutumia mpangilio maalum wa sauti kuundia vipashio vikubwa zaidi kwa mfano ,mofimu ,neno au maneno na sentensi.
Sapir (1921). Sapir anaieleza lugha kuwa ni mfumo ambao mwanadamu hujifunza ili autumie kuwasilisha mawazo, mahitaji na maoni yake kuhusu jambo Fulani katika mazingira yake. Sapir anasema kuwa mfumo huo hutumia ishara ambazo mtu huzitoa kwa hiari au kupenda kwake.
Trudgil(1974). Trudgil anasema kuwa lugha ni mfumo wa sauti za nasibu zinazotumiwa katika mawasiliano miongoni mwa watu wa jamii Fulani au kundi Fulani la watu katika jamii na ambao wana utamaduni wao. Trudgil anatambua utamaduni kama kigezo muhimu cha lugha.
TUKI (1990). Kamusi hii inasema kuwa lugha ni mfumo wa sauti zinazotumiwa na watu wa jamii Fulani wenye utamaduni uliosawa ama utamaduni ambao unafanana ili kuwasiliana.
Noam Chomsky(1977). Chomsky alieleza kuwa lugha ni mkusanyiko wa sentensi kila moja ikiwa na urefu Fulani na zinazoundwa kutokana na mkusanyiko wa viundio . hapa viundio vikiwa ni vitu kama vile silabi,ambazo huunda neno na neno uunda maneno mengi ambayo huwa sentensi moja ndefu kamilifu na yenye maana.
- lugha ni mfumo wenye kanuni, sheria na taratibu maalumu ambazo zinazowawezesha watumiaji wa lugha fulani kuwasiliana na kuelewana.
- lugha ni sauti zenye maana na ambazo zimikubaliwa na jamii kutumika katika mawasiliano.
- lugha ni mfumo wa sauti nasibu ambazo binadamu hutumia katika mawasiliano.
- Lugha ni utaratibu wa mfumo wa sauti za kutamkwa zenye maana zinazotumiwa na wanadamu kuwasiliana.