MATINI NI NINI?( WHAT IS A TEXT?)

 Ni wazo au mfululizo wa mawazo ambao unajitosheleza kimaana. Matini inaweza kuwa neno moja, kirai, kishazi, sentensi, aya, kifungu cha habari nk.

AINA ZA MATINI

Kuna aina mbili za matini ambazo ni :

·         Matini Chanzi/Chasili na

·          Matini Lengwa/matini tafsiri.

 Matini Chanzi/chasili (MC) “Source Text” ni matini ambayo yapo katika lugha yake ya awali au lugha yake iliyoandikiwa kabla ya mchakato wa kutafsiri.(translation process) · Matini Lengwa (ML) “Target Text” ni matini iliyotafsiriwa kutoka lugha yake iliyoandikiwa. Lugha Chanzi/Chasili (LC) ni lugha iliyotumika kuandikia matini chanzi (Source language) Lugha Lengwa (LL) (Target language) ni lugha iliyotumika kutafsiria matini chanzi au lugha unayoitumia kufanyia tafsiri. KISAWE/USAWE (EQUIVALENT/EQUIVALENCY) Katika muktadha wa tafsiri kisawe ni neno, kirai, kishazi, sentensi au hata maneno katika lugha lengwa ambayo maana na matumizi yake yanalingana au kukaribiana na yale ya neno, kirai, kishazi, sentensi au msemo mwingine katika lugha chanzi

Kwa ujumla tunaweza kusema kuwa, mfasiri ni mtu anayehamisha mawazo kutoka lugha moja (lugha chanzi) kwa kutumia lugha nyingine ili mawazo hayo yaeleweke na watu wasiojua au kuielewa lugha chanzi, na mawazo hayo sharti yawe katika maandishi.



MAREJEO

Cartford [1995] A linguistic Theory Translation

Mwansoko, H.J.M na wenzake [2006] Kitangulizi cha Tafsiri, Nadharia na

Mbinu.TUKI.Dar-es-salaam

Newmark, P [1982] Approaches to Translation, Oxford, Pergamon Press

Newmark, P [1988] A Text book of Translation, London, Prentice Hall.

Oxford University Press Dar-es-salaam

Semzaba, E [2006] Ngoswe, Penzi Kitovu cha Uzembe. The General Booksellers LTD.

D.S.M

TUKI [2002] Kamusi ya Kiswahili Sanifu. TUKI, Dar-es-salaam

TUKI [1985] Kiswahili, Jarida la Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili.

www.bakita.org.tz retrieved on Monday 04th July 2018

www.jim-mission.org.uk retrieved on Monday, 04th July 2018

www.ajol.inf retrieved on Monday, 04th July 2018

Vitabu vilivyotafsiriwa ambavyo vimetumika kama marejeo

Ayi Kwei Armah, Wema Hawajazaliwa, kimetafsiriwa na Abdilatif Abdalla

Ferdinand Oyono: House boy, Kimetafsiriwa na Raphael Khasao na Nathan Mwele.

William Shakespeare: Juliasi Kaizari: Kimetafsiria na Julius K. Nyerere

Mabepari wa Venisi: Kimetafsiriwa na Julius K. Nyerere

Hekaya za Abunuwasi: Kimetafsiriwa na Interterritorial Language Committee, East Africa

Alfu Lela Ulela: Kimetafsiriwa na Sir Richard Burton

Sir Rider Haggard: Mashimo ya Mfalme Suleiman

hati miliki zimehifadhiwa

Leave a Reply

scroll to top