Matumizi ya Nge- , ngeli- , ngali- , na -po-

Matumizi ya -nge-

Nge hutumika kuonyesha kwamba kitendo fulani hakijafanyika na kwa hivyo jambo fulani halijatokea lakini kuna uwezekano wa kufanya kitendo hicho na jambo hilo litokee.
Kiambishi -nge- kinapotumika mara mbili katika sentensi huwa na maana zifuatazo:

  • Wakati uliopo.
  • Huonyesha kuwa vitendo viwili havijatendeka.
  • Huonyesha masharti pale ambapo kitendo cha pili kinategemea kile cha kwanza ili
    kifanyike.
  • Huonyesha kuwa kuna uwezekano wa vitendo vyote viwili kutendeka.
    Mfano: Ningempiga angekufa
    Maana
    (i) Kuna uwezekano.
    (ii) Wakati uliopo.
    (iii) Kuna kutegemeana kwa vitendo vyote viwili.
    (iv) Vitendo vyote viwili havijatendeka.

Ni vyema kufahamu kuwa   ni makosa kutumia  –nge-  na –ngali- katika  sentensi  moja kwa sababu vyote ni viambishi ambavyo vinawakilisha wakati uliopita.

  • katika hali ya ukanushaji, ukanushaji wa – nge – ni – singe – na ule wa – ngali – ni – singali – .

Ukanushaji wa-nge-


Kiambishi -nge- kikikanushwa huwa namaana kuwa vitendo huwa vimefanyika
ambapo kiambishi si-huongezwa.
Mifano katika sentensi

Kuyakinisha – Angelia ningemsema.
Kukanusha – Asingelia nisingemsema.

Kuyakinisha – Angekula angeshiba.
Kukanusha – Asingekula asingeshiba

Kuyakinisha – Ungelala ungechelewa.
Kukanusha – Usingelala usingechelewa.

Kuyakinisha – Wangeitwa wangeitika.
Kukanusha – Wasingeitwa wasingeitika.

Kuyakinisha – Mngecheza vizuri mngeshinda
Kukanusha– Msingecheza vizuri msingeshinda.

Kuyakinisha – Ningemwita angekasirika.
Kukanusha – Nisingemwita asingekasirika.

Kuyakinisha – Tungeimba tungetuzwa.
Kukanusha – Tusingeimba tusingetuzwa.


Matumizi ya -ngeli-


Kiambishi -ngeli- kikitumiwa mara mbili katika sentensi huwa na maana zifuatazo:

  • Huonyesha kuwa jambo au mambo yaliyotajwa hayajatendeka. Hii ni kwa sababu wakati wa kutendeka kwa jambo au mambo haya umepita.
  • Huonyesha kuwa kuna uwezekano wa jambo au mambo yaliyotajwa kutendeka.
  • Huonyesha wakati uliopita.
  • Huonyesha hali ya masharti ambapovitendo viwili hutegemeana. Yaani, ni
    lazima kitendo cha kwanza kifanyike ili kile cha pili kifuate.
    Mfano katika sentensi
    Ningelisoma kwa bidii ningelifaulu vyema.
    Maana
    (i) Vitendo vyote viwili havijatendeka.
    (ii) Hakuna uwezekano wa vitendo vyote viwili kutendeka.
    (iii) Wakati uliopita.

Ukanushaji wa-ngeli-


Katika hali ya kukanusha -ngeli-, kiambishi -si- huongezwa na huonyesha kuwa vitendo
vilivyotajwa vimetendeka.

Kwa mfano;

Kuyakinisha: Ningelikuwa na pesaningeliwajengea wanafunzi wangu shule nzuri.
Kukanusha: Nisingelikuwa na pesanisingeliwajengea wanafunzi wangu shule nzuri

Kuyakinisha: Mngelisoma mngelimfika chuo kikuu.
Kukanusha: Msingelisoma msingelifika chuo kikuu

Kuyakinisha: Ungelinipiga ningelikushtaki.
Kukanusha: Usingelipiga nisingelishtaki.

Matumizi ya Ngali-


-ngali- ikitumika mara mbili katika sentensihuwa na maana zifuatazo:

  • Wakati uliopita.
  • Vitendo havitendeki au hakuna uwezekanowa vitendo husika kutendeka.
  • Hakuna matumaini.
  • Huonyesha masharti.
    Mfano katika sentensi
    Angalikuwa na uwezo angalinunua nyumba na kustarehe.
    Maana
    (i) Hakuwa na uwezo, hakununua nyumba
    na hakustarehe.
    (ii) Wakati uliopita.
    (iii) Hakuna uwezekano.
    (iv) Hakuna matumaini.
    ZINGATIA: -ngali- ikitumika mara moja katika sentensi huonyesha kuwa kitendo
    husika kiko katika hali ya kuendelea.

Matumizi ya kiambishi-po-


Kiambishi -po- kinaweza kutumiwa kuonyesha:
Wakati
Mifano katika sentensi: Anapoicheza watu hufurahia.,Alimapo huhema sana.

Ngombe anapokula nyasi huwa na afya nzuri.
Mahali
Mifano katika sentensi:
Alipouliwa pana matone ya damu., Palipojengwa nyumba panavutia.
Wanapochezea pana maji mengi., Ulipoanguka pana utelezi mkali.
Ukanushaji wa kiambishi -po-
Aghalabu kiambishi -po- hukanushwa kwa kuongewa-si-mwanzoni.
Mifano katika sentensi:
Kuyakinisha/Kukanusha

Mama aimbapo humfurahisha baba.- Mama asipoimba hamfurahishi baba.
Mtoto alapo hulala. – Mtoto asipokula halali.
Mimea hunawiri mvua inyeshapo. -Mimea hainawiri mvua isiponyesha.
Tuliapo hutokwa na machozi.- Tusipolia hatutokwi na machozi.

Leave a Reply

scroll to top