UTANGULIZI
Fonimu huchukuliwa kama kipashio kidogo zaidi cha sauti ambacho huweza kubainisha maana
katika maneno.kwa hivyo fonimu hapa huwa inakuwa foni inayotumikizwa katika lugha
mahususi.fonimu ndicho kipashio kidogo zaidi chenye kubainisha maana.fonimu huwa haina
maana kivyake lakini huchangia maana ya maneno.fonimu huwa na sifa ya ubainifu kwa sababu
hubainisha maana ya neno moja na linguine kwa mfano neno
i)Kanda na
tanda
sauti /k/ na /t/ katika (i) ndizo sauti zinazobainisha maana.sauti hizi basi ni sauti bainifu ambazo
ni fonimu.ubainifu huu hutokea kwa sababu tunapotumia sauti moja badala ya nyingine,maana
ya maneno au neno hubadilika.
Kwa upande mwingine alofoni ni matamshi mbalimbali ya fonimu moja au sura tofauti tofauti
za fonimu moja ambazo husababisha tofauti za maana.fonimu moja yaweza kutamkwa
kifonetiki kwa njia tofauti tofauti.Hutokea wakati ambapo fonimu moja inaweza kuwakilishwa
na zaidi ya sauti mbili zinazodhihirika kimatamshi,hizi tofauti za fonimu moja ndizo huitwa
alofoni.
Kwa mfano fonimu /a/ ya Kiswahili huwakilishwa na foni [ā] hata hivyo wakati mwingine /a/
huwakilishwa na vokali [ã] ya nasali.katika hali hii tunasema Kiswahili kina alofoni mbili za [ā]
yaani a kwa mfano katika neno mãmã na [ā]katika neno [sasa].
MBINU ZA KUTAMBUA FONIMU NA ALOFONI
a)mlingano wa kifonetiki
Hii ni dhana ambayo imezungumziwa na Hyman (1975) na Jones (1957) wanaelezea kuwa
alofoni za fonimu moja ambazo huonyesha mgawo wa kiutoano (hali ambayo sauti Fulani
hutokea katika mazingara Fulani na wala siyo mengine) lakini hazifanani kifonetiki haziwekwi
katika kundi moja.sauti zinazo fanana kifonetiki ni sauti zilizo na sifa bainifu zinazo fanana
Mgulu ( 2010 ) anaelezea kuwa kila lugha huteua baadhi ya sifa bainifu zinazotumiwa
kubainisha foni katika kiwango cha kifonetiki na wakazitumia katika kuzifafanua fonimu za
lugha yao.kulingana na Mweri(2010) anaeleza kuwa wakati mwingine hutokea hali ambapo
fonimu tofauti huonekana kama ambazo ni alofoni za fonimu moja.anatoa mfano wa kiingereza
akieleza kuwa sauti /ŋ/ na/h/huonekana kama ni alofoni za fonimu moja kwani/ŋ/ inapotokea
/h/haiwezi tokea.ansema kuwa hatuwezi kupata maneno yanayoishia kwa sauti /h/ katika
kiingereza,pia hakuna maneno yanayoanzia kwa sauti /ŋ/.kwa hali hii zinaonekana kama alofoni
za fonimu moja.kwa sababu sauti hizi zinakosa kufanana kifonetiki,fonimu hizi zinakua na sifa
zifuatazo;
-/h/ -isoguna
-Kikwamizi
– Glota
– Ya kinywa
/ŋ/ -guna
-kipasuo
-kaakaa laini
Ili sauti mbili ziwe alofoni za fonimu moja,ni sharti zifanane kifonetiki ili kuepukana na
uwezekano wa kuorodhesha sauti zozote kama alofoni za fonimu moja.
b)Mgawanyo wa kiutoano
katika mbinu hii,kitu ambacho kinazingatiwa ni ile hali ambayo sauti Fulani hutokea
katika mazingara Fulani na wala sio mengine.mbinu hii pia inatumika kubainisha sauti ambazo
ni fonimu au alofoni za lugha fulani.
R.S Mgulllu (2010) anaeleza kuwa fonolojia utoano ni dhana ambayo hutumiwa kuelezea
uhusiano uliopo baina ya sauti mbili za fonimu moja ambazo haziwezi kutokea katika mazingira
sawa,huku akimaanisha kuwa kila sauti ina mazingira yake maalumu ambayo hayawezi kukaliwa
na sauti nyingine.
Katika kitabu cha J.G Mweri (2010) utangulizi wa isimu. hali hii anaichukulia kama
mgawo kamilishani na kwa lugha ya Kiswahili anatupa mfano wa sauti/p/ ambayo inatamkwa
tofauti kutegemea na mazingara inamotokea anatoa mfano wa neno;
-/paka/
-/mpaka/
Katika maneno haya mawili,anasema kuwa neno /paka/ sauti /p/ hutamkwa na mpumuo
kidogo ilhali neno/mpaka /p/,hutamkwa bila mpumuo wowote. Aneleza kuwa mara nyingi /p/
inapotokea mwanzoni mwa neno au maneno katika Kiswahili hutamkwa na mpumuo,kwa
mfano neno [p h anya].na sauti hii inapotumika katika mazingara ya kati katika maneno
hutamkwa bila mpumuo wowote.anaelezea kuwa katika neno mpaka /p h /haiwezi kutokea
baada ya/m/.sauti /p/ na /p h / basi haziwezi kutokea katika mazingira sawa.
/p h /
P /p/ na /ph/ zinakua alofoni za fonimu moja ambayo ni[p]
/p/
c)Mpishano huru
mpishano huru ni hali mbayo sauti mbili zinaweza kutumika katika mazingira sawa bila ya
kubadilisha maana ya neno.kwa maneno mengine tunaweza kusema kuwa ni uhusiano wa
fonimu mbili tofauti kubadilishana nafasi moja katika maneno maalumu bila kubadili maana.
sauti hizi huwa tofauti kifonetiki na haziwezi kuwa alofoni za fonimu moja.sauti hizi
ambazo huwa tofauti kifonetiki huwa hazina ule uhusiano wa kiutoano,haziwezi kutumika
katika mazingira yale yale kwenye neno lakini sauti hizo ingawa ni tofauti hazisababishi tofauti
za maana katika maneno zinamotokea.
Kwa mfano; Angalau…………..angalao
Ramba…………….lamba
d)Jozi mlinganuo finyu
Jozi mlinganuo finyu ni mbinu ambayo inatumika kuzitambua fonimu za lugha. Mbinu
hii huwa ni hali ambayo maneno mawili katika lugha hutofautiana kwa sauti moja ambayo
hubainisha maana baina ya maneno hayo.sauti hizi huweza kutokea mwazoni mwa
maneno,katikati au hata mwishoni mwa maneno.kwa mfano;
-meno………………………neno
-kuni……………………….kumi
-kile………………………kila
Maneno ambayo yanahusika huwa lazima yawe na idadi sawa ya sauti na vile vile kila
neno ambalo linahusika liwe na mpangilio sawa wa sauti.katika hali hii basi ,ni kweli kusema
kuwa sauti mbili zinazo leta tofauti za kimaana katika maneno huwa ni kielelezo cha kifonetiki
cha fonimu mbili tofauti.
e)msawazisho changamano
Usawazisho hutokea pale ambapo sauti mbili tofauti katika lugha hupoteza tofauti zao hasa
katika mazingira Fulani katika neno.kwa mfano katika lugha ya Kiswahili usawazisho hujitokeza
katika neno ulimi.fonimu /l/ inatamkwa kama [d] inapotanguliwa na nazali ya ufizi /n/.kwa
hivyo neno hili ulimi(umoja) ndimi (wingi) /n/ hapa basi /l/ ndilo umbo
ndani na hubadilika katika mazingira inapotanguliwa na /n/ hali hii huwakilishwa kwa mchoro
hivi;
[l] [d]/n katika hali hii inamaanisha kuwa /l/ inageuka na kuwa
[d] katika umbo nje.
Marejeleo.
J.Habwe,P.karanja (2004)misingi ya sarufi ya Kiswahili phoenix publishers Ltd Nairobi.
J.Mweri (2010) utangulizi wa wa isimu
R.S Mgullu mtalaa wa isimu fonetiki,fonolojia na mofolojia ya Kiswahili Autolitho Ltd Nairobi.