Kiima ni neno au kifungu cha maneno katika sentensi ambacho hutangulia kitenzi na aghalabu huonyesha mtenda.Kiima huonyesha nomino au kiwakilishi ambacho hufanikisha kutendeka kwa kitendo.
Miundo ya kiima
Nomino pekee
Junet anapika ugali.
Ng’ombe anakula nyasi.
Cherop anasoma habari.
Nomino,kiunganishi na nomino
Duma na mbwa wemefungiwa pamoja.
Wanafunzi na walimu wanasoma magazeti.
Nomino na kivumishi
Mtoto yule anapenda kandanda.
Datari huyo anatibu wagonjwa
Kiwakilishi
Hao wanaimba nyimbo za mapenzi.
Yule atasafiri kesho.
Kiwakilishi na kivumishi
Yule mtundu amefukuzwa shuleni.
Yale mengi yamevunwa.
Nomino na kishazi tegemezi
Muuguzi aliyewatubu wagonjwa jana amefutwa kazi.
Tanbihi: Kiima chaweza kutokea katika sehemu yoyote ya sentensi.