Mofimu ni Kipashio Kidogo zaidi cha neno chenye maana kisarufi.Pia, mofimu inaweza fasiriwa kuwa ni kipashio kidogo katika lugha ambacho hakiwezi kugawika zaidi bila kupoteza maana yake ya kisarufi. Kuna aina mbili kuu ya mofimu;
- Mofimu huru
Mofimu huru ni aina ya mofimu ambayo huweza kusimama peke yake na kujitosheleza kimaana yaani huwa na sifa ya neno. Mfano; mama, Baba, Dada, Kaka, Mjomba, Shangazi leo,simu,meza,peremende,karatasi,darasa,hukumu,jaji,picha n.k. Kwa mifano hiyo utagundua kuwa mofimu huru haziwezi kugawanyika zaidi na kubeba maana kisarufi, kwa maana kwamba mofimu ‘kaka’ ikigawanywa ka-ka, ‘ka’ hii haina maana yoyote kisarufi zaidi ya kuwa silabi.Aghalabu mofimu huru huwa nomino, vivumishi au vielezi visivyochukua viambishi vya ngeli.
- Mofimu tegemezi
Mofimu tegemezi ni aina ya mofimu ambayo huweza kuvunjwavunjwa na kubeba maana kisarufi, mofimu tegemezi hutegemeana ili kuleta maana kamili ya neno.
Mfano; neno ‘anasoma’ limeundwa na mofimu zifuatazo:- [a-na-som-a] ambazo kila moja hubeba dhana Fulani ya kisarufi.
dhana hizo za kisarufi ni kama vile:
Dhana ya kisarufi /mofimu | mfano |
Mzizi (Sehemu ya neno inayobeba maana kuu na isiyoweza kubadilishwa) | M- tu, som-a, andik-a, n.k. |
Nafsi | Lilianguka.Yalianguka. |
Ngeli | KimevunjikaLinatembea |
Kikanushi | SikumpigaHalijaoza. |
Njeo/wakati | Liliiva.Analia.Tutaimba.Alipoenda. |
Hali | Me, nge, ngali, hu, ki, ka, n.k. |
Mahali | Alipoingia.Alikoingia.Alimoingia. |
Mtendwa/watendwa/kitendwa/vitendwa/shamirisho | Alijikata.Alichikichukua.Kilichowaua. |
Mnyambuliko/kauli | Alimpigia.AlimliliaAlinikosea. |