Muundo wa sentensi sahili unaweza kuonyeshwa kwa kuipambanua. Kuipambanua sentensi sahili ni kuonyesha aina za maneno yaliyoiunda. Ili kuonyesha muundo wa sentensi sahili, ni muhimu kwanza kuangazia maana ya kikundi nomino (KN) na kikundi tenzi (KT).
Kikundi nomino (KN)
Kikundi nomino ni sehemu ya sentensi ambayo huundwa na nomino au kiwakilishi, na pengine pamoja na kivumishi, kiunganishi na kielezi lakini bila kitenzi.
Kikundi tenzi (KT)
Kikundi tenzi ni sehemu Photo editors a phone ya sentensi ambayo huundwa na kitenzi pekee, au kitenzi pamoja na kielezi, kihusishi na hata wakati mwingine nomino.
Mifano katika sentensi:
1. Moraa mpole mwerevu sana amepita mtihani vizuri.
Kikundi nomino: Moraa mwerevu sana.
Kikundi tenzi: A tunemepita mtihani vizuri.
2. Moses ni mkimbiaji hodari sana.
Kikundi nomino: Moses
Kikundi tenzi: ni mkimbiaji hodari sana.
3. Paka mweusi sana amemla panya leo asubuhi.
Kikundi nomino: Paka mweusi sana .
Kikundi tenzi: amemla panya leo asubuhi.
4. Yeye na mimi tutasafiri ulaya jumatatu.
Kikundi nomino: Yeye na mimi.
Kikundi tenzi: tutasafiri ulaya jumatatu.
5. Gari lake ndogo linaendishwa na babake.
Kikundi nomino: Gari lake ndogo.
Kikundi tenzi: linaendishwa na babake.