Ngeli ya A- WA
Nomino katika ngeli hii huchukua kiambishi a-umoja na wa-wingi ili kuleta upatanisho wa kisarufi. Nomino katika ngeli hii ni zile zinazotaja viumbe wote. Hujumuisha majina ya watu, wanyama, ndege, samaki na hata wadudu. Mifano ya nomino katika ngeli hii ni malaika, askofu, binamu, kipofu, vyura, samaki, ndege, mamba, kaa, siafu n.k
Huchukua miundo kama vile M-WA, M-MI, KI-VI, n.k.
Zingatia: Miundo ya nomino katika ngeli ina maana ya viambishi vya umoja na wingi katika nomino husika
Ifuatayo ni mifano ya nomino zinazopatikana katika ngeli ya A- WA
- mtu-watu,
- mkulima-wakulima
- mtume-mitume
- mkizi-mikizi
- kiwete-viwete
- kibyongo-vibyongo
- nabii-manabii
- kuku-kuku
- Waziri-Mawaziri
Miundo ya nomino za ngeli ya A-WA
Ki -Vi kwa mfano kipepeo – Vipepeo
M- Mi kwa mfano Mkizi – Mikizi
M – Mw – Wa kwa Mfano Mtu – Watu Mwalimu – Walimu
Ch – Vy kwa mfano chura – Vyura
Tanbihi: Ngeli ya A-WA hujumuisha nomino zinazochukua kiambishi ma katika wingi, kwa mfano daktari- madaktari na vile vile hujumuisha nomino ambazo hazibadiliki katika umoja na wingi kwa mfano samaki, punda n.k.
Ngeli za Nomino |
Ngeli ya U-I |
Ngeli ya U-ZI |
Ngeli ya YA-YA |
Ngeli ya I-I |
Ngeli ya U-U |
Ngeli ya LI-YA |
Ngeli ya U-YA |
Ngeli ya KI-VI |
Ngeli ya KU-KU |
Ngeli ya I-ZI |
Ngeli ya PA-KU-MU |