Nomino katika ngeli hii huchukua kiambishi I katika umoja na kiambishi ZI katika wingi ili kuleta upatanisho wa kisarufi.

Mifano ya nomino katika ngeli hii ni:

  • Yumba
  • Baiskeli 
  • Karatasi
  • Redio  
  • Meza 
  • Dini
  • Dawa
  • Ndizi
  • Jozi

Nomino katika ngeli hii hazibadiliki katika umoja na wingi.

UmojaWingi
Ndizi imeivaNdizi zimeiva
Shule imefungwaShule zimefungwa
Baiskeli imepoteaBaiskeli zimepotea
Karatasi imeandikwaKaratasi zimeandikwa
Ngeli za Nomino
Ngeli ya A-WA
Ngeli ya U-I
Ngeli ya U-ZI
Ngeli ya YA-YA
Ngeli ya I-I
Ngeli ya U-U
Ngeli ya LI-YA
Ngeli ya U-YA
Ngeli ya KI-VI
Ngeli ya KU-KU
Ngeli ya PA-KU-MU