Nomino katika ngeli hii huchukua kiambishi Ki – katika umoja na Vi- katika wingi. Huhusisha majina ya vifaa, sehemu za mwili, vitu, udogo au kudunisha, lugha, n.k.

Mifano ya nomino katika ngeli hii ni;

  • kisu-visu
  • kitabu-vitabu
  • chakula-vyakula
  • chanda-vyanda
  • kijitu-vijitu
  • kigombe-vigombe 
  • kiguu-viguu
  • kidovu-vidovu
UmojaWingi
Kiuno kimenenguliwaViuno vimenenguliwa
Kitoto kilichapwaVitoto vilichapwa
Cheti kilipeanwaVyeti vilipeanwa
Chuo kimefunguliwaVyuo vimefunguliwa
Muundo wa Ngeli ya Ki -Vi

Nomino za ngeli hii huanzia kwa kiambishi KI au CH katika umoja na kuchukua viambishi VI au VY katika wingi. Huhusisha vitu visivyokuwa na uhai. kwa mfano;

KI- VIKiti –viti

CH- VYChakula – Vyakula

Ngeli za Nomino
Ngeli ya A-WA
Ngeli ya U-I
Ngeli ya U-ZI
Ngeli ya YA-YA
Ngeli ya I-I
Ngeli ya U-U
Ngeli ya LI-YA
Ngeli ya U-YA
Ngeli ya KU-KU
Ngeli ya I-ZI
Ngeli ya PA-KU-MU