Nomino katika ngeli hii huchukua kiambishi cha umoja LI na cha wingi YA ili kuleta upatanisho wa kisarufi.Huwa na majina ya sehemu za mwili, dhana, vifaa, nomino zilizo katika hali ya ukubwa n.k. Mifano ya nomino zipatikanazo katika ngeli hii ni;
- jicho-macho
- jina-majina
- jitu-majitu
- goma-magoma
- jambo-mambo
- janga-majanga
- jembe-majembe
- jeneza-majeneza
- wazo-mawazo
- tunda-matunda
- jua-majua
- ziwa-maziwa
- ua-maua
Umoja | Wingi |
Dirisha limefunguliwa | Madirisha yamefunguliwa |
Jiwe limevunjika | Mawe yamevunjika |
Gari limeegeshwa kando ya barabara | Magari yameegeshwa kando ya barabara |
Dege limepaa | Madege yamepaa |
Nomino za ngeli hii huchukua miundo tofauti tofauti katika hali ya umoja na wingi;
JI- MA kwa mfano jifya – mafya
JA- MA kwa mfano Jani – Majani
JI – ME kwa mfano Jino- Meno
MA – Mashati, madege n.k.
Ngeli za Nomino |
Ngeli ya A-WA |
Ngeli ya U-I |
Ngeli ya U-ZI |
Ngeli ya YA-YA |
Ngeli ya I-I |
Ngeli ya U-U |
Ngeli ya U-YA |
Ngeli ya KI-VI |
Ngeli ya KU-KU |
Ngeli ya I-ZI |
Ngeli ya PA-KU-MU |