Ngeli hii huitwa ngeli ya mahali. Huitwa ngeli ya mahali kwa sababu hujumuisha nomino moja tu ambayo ni ya mahali. Kimuundo nomino hii ya mahali hubadilika katika umoja na wingi. Ngeli ya mahali hugawanyika katika vikundi vitatu ambavyo hutegemea viambishi awali vya upatanisho wa kisarufi ambavyo ni PA – KU -MU
- PA (mahali karibu au panapodhihirika) k.m. Kitabu kipo pale.
- KU (mahali mbali au kusikodhihirika) k.m. Mahali kule kunafaa.
- MU (ndani ya) k.m. Mahali mle mna siafu.
Tanbihi: Ni kosa kuchanganya viambishi hivi katika sentensi moja.
Ngeli za Nomino |
Ngeli ya A-WA |
Ngeli ya U-I |
Ngeli ya U-ZI |
Ngeli ya YA-YA |
Ngeli ya I-I |
Ngeli ya U-U |
Ngeli ya LI-YA |
Ngeli ya U-YA |
Ngeli ya KI-VI |
Ngeli ya KU-KU |
Ngeli ya I-ZI |