Nomino katika ngeli hii huchukua kiambishi awali U katika umoja na I katika wingi ili kuleta upatanisho wa kisarufi.Huhusisha majina ya mimea, sehemu za mwili, vifaa, matendo, maumbile, n.k.

Mifano ya nomino zinazopatikana katika ngeli hii ni;

  • Mchungwa-michungwa
  • Mkoko-mikoko
  • mkono-mikono
  • mfupa-mifupa
  • msumari-misumari
  • mgomo-migomo
  • mwendo-myendo
  • msukosuko-misukosuko
  • mlima-milima
  • mwamba-myamba
UmojaWingi
Mfupa huu UmevunjikaMifupahii imevunjika 
 Msumari huu utatumiwaMisumari hii itatumiwa 
 Msukosuko huu umehiaribu nchi misukosuko hii imehiaribu nchi

Miundo ya nomino za ngeli ya U- I

Mw – Mi kwa mfano mwavuli – Miavuli

M – Mi kwa mfano Mlima – Milima

Ngeli za Nomino
Ngeli ya A-WA
Ngeli ya U-ZI
Ngeli ya YA-YA
Ngeli ya I-I
Ngeli ya U-U
Ngeli ya LI-YA
Ngeli ya U-YA
Ngeli ya KI-VI
Ngeli ya KU-KU
Ngeli ya I-ZI
Ngeli ya PA-KU-MU