Nomino katika ngeli hii huchukua kiambishi cha umoja U na kile cha wingi YA ili kuleta upatanisho wa kisarufi.Huhusisha majina ya hali, matendo,baadhi ya nomino za dhahania n.k. Mifano ya nomino katika ngeli hii ni;
- Ugonjwa-magonjwa
- upana-mapana
- uasi-maasi
- uchungu-machungu
- ulezi-malezi
- uovu-maovu
- uhusiano-mahusiano
Umoja | Wingi |
Ugonjwa ulimwangamiza | Magonjwa yaliwaangamiza |
Upana unaofaa wa chumba | Mapana yanayofaa ya vyumba |
Upishi unapendeza | Mapishi yanapendeza |
Ulezi unaofaa | Malezi yanayofaa |
Nyingi za nomino katika ngeli hii ya U- YA huchukua kiambish U katika umoja na MA katika wingi.Kwa mfano Uasi – Maasi, Upishi – Mapishi, Ugonjwa – Magonjwa
Ngeli za Nomino |
Ngeli ya A-WA |
Ngeli ya U-I |
Ngeli ya U-ZI |
Ngeli ya YA-YA |
Ngeli ya I-I |
Ngeli ya U-U |
Ngeli ya LI-YA |
Ngeli ya KI-VI |
Ngeli ya KU-KU |
Ngeli ya I-ZI |
Ngeli ya PA-KU-MU |