Nomino katika ngeli hii huchukua kiambishi awali U katika umoja na kiambishi ZI katika wingi ili kuleta upatanisho wa kisarufi.

  • wayo-nyayo
  • wakati-nyakati
  • uso-nyuso
  • ufa-nyufa
  • ufunguo-funguo
  • ufagio-fagio
  • wembe-nyembe
  • uwanja-nyanja
  • ujumbe-jumbe
  • ukoo-koo
  • waraka-nyaraka
  • waya-nyaya
UmojaWingi
Ufagio ulionunuliwa na mama umepoteaFagio zilizonunuliwa jana na mama zimepotea
Waraka umeadikwa na mwanafunziNyaraka zimeandikwa na wanafunzi
Wembe umemkata mtotoNyembe zimewakata watoto
Ufunguo wa nyumba umepoteaFunguo za nyumba zimepotea

Nomino katika ngeli hii huchukua miundo ifuatayo;

W-NY – Wayo – Nyayo, wembe – Nyembe

U-NY, – Unyasi – Nyasi

U-F, – Ufagio – Fagio

U – ND – Udevu – Ndevu, Ulimi – Ndimi

Ngeli za Nomino
Ngeli ya A-WA
Ngeli ya U-I
Ngeli ya YA-YA
Ngeli ya I-I
Ngeli ya U-U
Ngeli ya LI-YA
Ngeli ya U-YA
Ngeli ya KI-VI
Ngeli ya KU-KU
Ngeli ya I-ZI
Ngeli ya PA-KU-MU