Nomino katika ngeli hii huchukua kiambishi cha umoja YA na cha wingi YA ili kuleta upatanisho wa kisarufi.Aghalabu nomino zake hujumuisha vitu visivyohesabika hasa vitu vyoevu.nomino katika ngelihii hazibadiliki katika umoja na wingi. baadhi ya nomino hizo ni;

  • manukato  
  • mauti
  • maziwa  
  • marashi
  • mahubiri   
  • majira
  • maradhi
  • maafa
  • mazingira
UmojaWingi
Manukato yananukiaManukato yananukia
Maziwa yamemwagikaMaziwa yamemwagika
Maringo yanakeraMaringo yanakera
Mafuta yamemwagikaMafuta yamemwagika

Miundo ya nomino za Ngeli ya YA- YA

Nomino za ngeli hii hazibadiliki katika umoja na wingi. Nyingi huchukua kiambishi MA katika umoja na wingi. kwa mfano manukato – manukato, mafuta- mafuta, maziwa – maziwa.

Ngeli za Nomino
Ngeli ya A-WA
Ngeli ya U-I
Ngeli ya U-ZI
Ngeli ya I-I
Ngeli ya U-U
Ngeli ya LI-YA
Ngeli ya U-YA
Ngeli ya KI-VI
Ngeli ya KU-KU
Ngeli ya I-ZI
Ngeli ya PA-KU-MU